LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Mkuu afunga Maonesho ya Teknolojia ya Dhahabu Geita

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameahirisha Maonesho ya Teknolojia ya Uzalishaji Dhahabu kwa Maendeleo ya Kijamii na Uchumi wa Viwanda mkoani Geita kwa kuwahimiza wachimbaji wadogo kuunda vikundi ili kunufaika na mikopo inayotolewa na mabenki nchini kupitia dhamana ya Benki Kuu (BOT) kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao.

Aidha ameagiza fedha za maendeleo ya jamii zinazotolewa na makampuni ya uchimbaji madini nchini kufanya kazi iliyokusudiwa ambapo ameupongeza Mkoa Geita kwa kutumia vyema fedha hizo kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo afya, barabara na soko la kisasa.

Mhe. Majaliwa aliahirisha maonesho hayo jana Septemba 30, 2018 huku akitoa ridhaa ya kuendelea hadi kesho kutwa jumatano kufuatia ombi la Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Robert Gabriel. Maonesho hayo yalianza Septembe 24, 2018 katika viwanja vya CCM Kalangalala Mjini Geita na kushirikisha zaidi ya makampuni 250 nchini.
Awali viongozi mbalimbali mkoani Geita wakimlaki Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika uwanja wa ndege wa GGM
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto), akisalimiana na Naibu Waziri wa Madini Mwl. Doto Biteko (kulia) alipowasili mkoani Geita.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto), akisalimiana na mbunge wa Geita Mjini Costantine Kanyasu (kulia) alipowasili mkoani Geita.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto), akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili uwanja wa ndege
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwasikiliza baadhi ya washiriki wa Maonesho ya Teknolojia ya Uzalishaji Dhahabu kwa Maendeleo ya Kijamii na Uchumi wa Viwanda mkoani Geita, alipokuwa akitembelea mabanda
Tazama hapa chini BMG Online Tv

No comments:

Powered by Blogger.