Mwanza wapania kuendeleza mchezo wa kikapu
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Matangazo.
Judith Ferdinand, BMG
Wadau
mbalimbali mkoani Mwanza wametakiwa kuendeleza
mchezo wa mpira wa kikapu (Basketball ), ili kuibua na kuendeleza vipaji vipya
kutoka kwa vijana na kuuwakilisha mkoa katika mashindano mbalimbali ya kitaifa
na kimataifa.
Mratibu wa
Mpira wa Kikapu kwa watoto na vijana mkoani Mwanza, Bahati Kizito alitoa rai
hiyo kwenye bonanza la mchezo huo lililoshirikisha shule za msingi na sekondari
kutoka Nyamagana, Ilemela na Magu.
Kizito
alisema, licha ya mafanikio walioyapata katika mchezo huo bado wanakabiliwa na
upungufu wa vifaa pamoja na viwanja hivyo anaomba wadau kuwaunga mkono na
kuendeleza mpira wa kikapu kwa kusaidia kutatua changamoto hizo.
Alisema,
bonanza hilo ni sehemu ya programu ya uibuaji na uendelezaji wa mchezo huo,
ambayo ipo katika baadhi ya mikoa nchini ikiwa chini ya mpango uitwao “Tanzania
Youth Basketball Program”.
Pia alisema baada
ya bonaza hilo, nguvu itaelekewa kwa wachezaji walioshiriki kuendelea na
mazoezi kila siku baada ya muda wa masomo katika viwanja vilivyo karibu na
maeneo wanayoishi ikiwemo Kiloleli, Mirongo, B.O.T, Pasiansi, Butimba TTC na
Kirumba ambapo kutakuwa na makocha watakaokuwa wakiwafundisha ili kuwaimarisha
zaidi.
Naye mbunge
wa Nyamagana , Stanslaus Mabula ambaye
alikuwa mgeni rasmi kwenye bonanza hilo alisema michezo ni afya na ajira hivyo
washiriki watumie nafasi hiyo vizuri,
huku jitihada za kuboresha miundombinu ya viwanja katika maeneo ya Sabasaba na
Pamba zikiendelea.
Kwa upande
Katibu na mwakilishi wa mbunge wa Ilemela Kanda ya Bugogwa, Rebeca Yusuph alisema
mbunge wa jimbo hilo yuko tayari kushirikiana na wadau wa mchezo huo ili
kuhakikisha wanaibua na kuendeleza vipaji vya vijana.
Katika
bonanza hilo, timu ya wasichana kutoka
shule ya J-Mond iliibuka na ushindi dhidi ya Kiloleli huku wavulana Kiloleli ikiichapa
Thaqaafa goli 10-8.
No comments: