Ukosefu wa vyoo wahatarisha afya za wavuvi wilayani Ilemela
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Afisa
Mfawidhi wa Ulinzi wa Raslimali za Uvuvi Kanda Kuu ya Ziwa Victoria, Didas
Mtambalike akizungumza na wananchi pamoja na wavuvi wa mwalo wa Bwiru  Kijiweni wilayani Ilemela.
Judith  Ferdinand, Mwanza
Afisa
Mfawidhi wa Ulinzi wa Raslimali za Uvuvi Kanda Kuu ya Ziwa, Victoria Didas
Mtambalike ameunda kamati maalum ambayo itasimami ujenzi wa choo katika Mwalo
wa Bwiru  Kijiweni uliopo wilaya ya
Ilemela mkoani Mwanza.
Hii ni
kutokana na  wakazi wa mwalo huo  kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa choo
kwa muda mrefu na hivyo kulazimika kujisaidia katika maeneo  ambayo siyo rasmi na kuhatarisha afya zao.
Mtambalike
alilazimika kuunda kamati hiyo baada ya wananchi wa maeneo hayo  kulalamikia ukosefu wa choo kwa muda mrefu
wakati akizungumza nao kwenye mkutano uliofanyika mwaloni hapo sanjari na
kutumia fursa hiyo kuagiza kamati hiyo kufanya utafiti wa eneo lipi ambalo
linafaa kwa ujenzi nje ya mita sitini kutoka ziwani.
Pia
Mtambalike alitumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi wa maeneo hayo kuanzisha
ushirika wa wavuvi  katika mwalo huo ili
uweze kuwasaidia katika masuala mbalimbali ikiwemo kujiinua kiuchumi.
Naye  Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Manispaa  ya Ilemela, Musa Mukonga alisema halmashauri
hiyo inaendelea kuimarisha miundombinu 
katika mialo yote ambapo imetenga shilingi milioni 300 kwa ajili ya
kufanya maendeleo kwenye sekta ya uvuvi.

No comments: