Unaweza kuwa na chakula kingi lakini ukawa na njaa- Dkt. Tizeba
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akisisitiza
jambo wakati akizungumza jana Oktoba 11, 2018 kwenye kongamano maalumu la
muelekeo wa siku ya chakula Duniani katika ukumbi wa mihadhara (MLT 9) katika
Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo-SUA Mkoani Morogoro.
Waziri
wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza
kwenye kongamano maalumu la muelekeo wa siku ya chakula Duniani katika ukumbi
wa mihadhara (MLT 9) katika Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo-SUA, Mkoani
Morogoro.
Waziri
wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi
shahada za awali Chuo kikuu cha Sokoine Bi Suzan Agustino wakati alipowasili
kushiriki kongamano maalumu la muelekeo wa siku ya chakula Duniani katika
ukumbi wa mihadhara (MLT 9) katika Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo-SUA.
Waziri
wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Kushoto) akikagua Shamba la mafunzo ya
Mazao ya kipaumbele (Pamba, Kokoa, Kahawa, Chai, Katani, Miwa na Matunda kabla
ya kushiriki kongamano maalumu la muelekeo wa siku ya chakula Duniani.
Na
Mathias Canal, WK-Morogoro
Utamaduni
wa kula aina fulani ya chakula kwa aina moja tu ni miongoni mwa mambo
yanayowafanya wananchi kukumbwa na njaa pindi kinapokosekana aina ya chakula
kile walichokizoea.
Moja ya
matatizo makubwa katika jamii ni pamoja na wananchi kuamini katika utamaduni wa
aina moja ya chakula jambo ambalo halipaswi kutiliwa mkazo kwa namna yoyote.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba Leo tarehe 11
Octoba 2018 wakati akizungumza kwenye mdahalo wa kuelekea siku ya chakula Dunia
ambayo hafla ya kilele chake itafanyika Mjini Tunduma Mkoani Songwe tarehe 16
Octoba 2018.
Katika
mdahalo huo ulioandaliwa na Shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa
umoja wa chakula Duniani (FAO), Mpango wa chakula wa umoja wa Mataifa (WFP), Benki
ya Kimataifa ya Maendeleo ya kilimo (IFAD) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha
Kilimo cha Sokoine, Waziri Tizeba alisema kuwa katika kipindi hichi Kilimo cha
kujikimu sio mjadala serikalini na nchi kwa ujumla bali serikali inaendelea na
juhudi za makusudi kusisitiza kilimo cha biashara ili wananchi waondokane na
umasikini wa kipato.
"Na
katika hali ya kawaida endapo utekelezaji wa mpango wa kuendeleza sekta ya
kilimo awamu ya pili (ASDP II) ukitekelezwa ipasavyo nchi ya Tanzania kabla ya
kufikia mwaka 2025 itafikia uchumi wa kati" Alikaririwa Dkt Tizeba na
kuongeza kuwa; "Ni
lazima tusisitize wakulima kushughulika na kilimo biashara ili waweze kumudu
elimu bora, afya bora na kila kitu".
Alisema
kuwa njaa haijalishi kile kinachozalishwa bali njaa ni umasikini unaosababishwa
na kutokuwa na uwezo wa kupata chakula kwani kuna uwezekana mwananchi
asizalishe chakula lakini akawa na uwezo wa kununua chakula chochote
anachotaka.
Alisema
kuwa serikali imeanza mkakati madhubuti wa kuimarisha masoko ya mazao
mbalimbali ndani ya nchi sambamba na kuimarisha masoko ya nje ambapo katika
Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) muhimili wa tatu
ni kuboresha masoko.
“ Ndugu
zangu sio kwamba hatuna chakula wakati mwingine chakula kipo lakini watu hawali
vizuri kutokana na mila na tamaduni zetu za kiafrika ambapo kwa wakati wote
wanawake ndio wapishi na wanaume kusalia kuwa wahemeaji (Kununua).
Kwa
upande wake Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo (Utawala na
Fedha) Prof Yonika Ngaga ametoa pongezi kwa waziri wa kilimo Mhandisi Dkt
Charles Tizeba kwa kukubali kushiriki mdahalo huo ambao mjadala mkubwa ulihusu
kujadili namna bora ya kutatua changamoto ya njaa nchini Tanzania na Barani
Afrika kwa ujumla wake.
No comments: