Header Ads

Wamiliki wa leseni Mererani watakiwa kulipa madeni yao

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Naibu Waziri wa Madini Mwl. Doto Mashaka Biteko amewataka baadhi ya wamiliki wa leseni za uchimbaji madini katika machimbo ya Mererani mkoani Manyara kulipa madeni yote wanayodaiwa na serikali kabla ya kukimbilia katika maeneo mengine na kuomba leseni nyingine za uchimbaji.

Mwl. Biteko aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na wachimbaji wa madini ya vito (Ruby) katika machimbo ya Kitwai A, wilayani Simanjiro ambapo alisema zaidi ya leseni 200 zimeombwa katika eneo hilo na wengi wa walioomba wametoka Mererani.

SOMA>>>Mwekezaji Simanjiro atakiwa kutoa mikataba kwa wafanyakazi

No comments:

Powered by Blogger.