Waziri wa Kilimo azuia Halmashauri kutoa vibali vya ununuzi wa Kahama
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles
Tizeba (Mb) akitangaza zuio la Halmashauri kutoa vibali vya kununua kahawa
wakati akihutubia maelfu ya wanachi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara
uwanja wa Changarawe Wilayani Karagwe kwenye muendelezo wa ziara ya Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) aliyoianza Jana
tarehe 6 Octoba 2018 mkoani Kagera.
Na Mathias Canal-WK, Karagwe-Kagera
Waziri wa
kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) amezuia Halmashauri zote nchini
kujihusisha na utoaji wa vibali kwa wafanyabiashara vya kununua kahawa kwa
wakulima.
Dkt Tizeba
ametoa zuio hilo Leo tarehe 7 Octoba 2018 wakati akihutubia maelfu ya wanachi
waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uwanja wa Changarawe Wilayani Karagwe
wakati wa muendelezo wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Kassim Majaliwa (Mb) aliyoianza Jana tarehe 6 Octoba 2018 mkoani Kagera.
"Wafanyabiashara
wa kahawa ili wanunue zao hilo walikuwa wanaenda kuomba kibali cha ununuzi
kilichokuwa kinatolewa na Halmashauri za wilaya, Hili jambo tumelitafakari na
wenzangu wa Wizara hususani watendaji pamoja na Bodi ya kahawa tumeona halina maana
tena" Alikaririwa Dkt Tizeba
Waziri
Tizeba alisema kuwa Wafanyabiashara hawana sababu ya kuomba vibali kwenye
Halmashauri vya kununua kahawa badala yake itatosha kuwa na leseni ya biashara
ya Kahawa inayotolewa na Bodi ya Kahawa Tanzania, jambo ambalo linawatambulisha
wafanyabiashara kwamba wanalipa kodi.
"Sasa
hivi tunaingia kwenye mfumo wa ushirika hivyo Wafanyabiashara watanunua kahawa
kupitia mfumo huo mahususi hivyo hakuna sababu ya kusumbuliwa na Halmashauri
kwa kupewa vibali" Alisisitiza
Aidha, Kuhusu
kahawa ya madaraja ya chini, Waziri Tizeba alisema kuwa kahawa hiyo kwa kipindi
kirefu imekuwa ikizuiliwa kuuzwa nje ya nchi. Hivyo kwa mujibu wa utafiti wa
kubaini namna inavyotumika nchini ilibainika kuwa kahawa hiyo inanunuliwa na
watu wachache ambao ndio wanaratibu utaratibu wa kuuza nje huku waliokoboa
wakizuiwa kuuza nje.
"Jambo
hili sio sawa, sisi tunachotaka wakulima washiriki kwenye mnyororo wa thamani
utakaowafanya wawe na uwezo wa kutafuta mnunuzi nchini au nje ya nchi
watakapopewa bei nzuri" Alisema.
Dkt Tizeba
aliongeza kuwa Kahawa hiyo itauzwa popote Duniani kutegemea na kiasi cha fedha
kitakachokuwa rafiki na chenye tija kwa mkulima.
No comments: