LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wadau wajadili namna ya kupambana na watoto wanaoishi Mitaani

Wasiliana na BMG Blog/ BMG Online TV kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.
Kibwagizo kutoka Chama cha Waalimu Tanzania (CWT).

Judith Ferdinand, BMG
Ili kupambana na changamoto ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu Jijini Mwanza, Sirekali imetakiwa kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na asasi na mashirika binafsi.

Akizungumza katika kikao kazi cha wadau na watendaji wa Serikali kilichoandaliwa na Shirika la Railway Children Africa (RCA), Mkurugenzi wa shirika hilo Mussa Mgata alisema ni vyema mkakati wa pamoja ukaandaliwa katika wilaya zote za mkoa wa Mwanza unaohusu masuala ya watoto hususani wanaoishi mitaani ambao utasaidia kupambana na changamoto hiyo.

Mgata alisema viongozi wa Serikali za wilaya na mkoa wanapaswa kwenda katika maeneo wanayoishi watoto na vijana wanaofanya kazi na kuishi mtaani ili kujionea hali halisi ya mazingira na changamoto wanazokutana nazo.

Alisema shirika Railway Children Africa (RCA) limefanya miradi mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia watoto na vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi ambapo tangu Oktoba 2017 hadi Septemba 2018 limewafikia wanufaika 1,141 ambapo 125 walikuwa kwenye dharura ya kuhitaji msaada, 691 katika huduma za matibabu, 169 kuwarudisha kwenye familia zao, 507 kuwasaidia vifaa vya shule, 306 kuwarudisha na kuwaandikisha shuleni pamoja na 443 kuwapa mafunzo ya stadi za maisha. 

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dkt. Severine Lalika alikiri kwamba Serikali haiwezi kufanya kazi ya maendeleo pekee bila kushirikisha sekta binafsi hivyo kwa kutambua umuhimu wa kazi inayofanywa na shirika hilo, ipo tayari kushirikiana pamoja na kuwa karibu nalo, kwani kazi wanayoifanya ya kusaidia watoto wanaoishi mitaani, kuwakusanya sanjari na kuwarudisha katika familia zao ni nzuri na ya kujivunia katika kuboresha maendeleo ya vijana wa taifa la kesho.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,  John Wanga alisema ili kumaliza tatizo hilo inapaswa kutafuta namna ya kuzuia watu ambao ni wasamaria wema wanaowapatia msaada wa fedha kwani hatua hiyo inawafanya waendelee kuwepo mitaani. Alisema ni vyema kuweka kambi maalum kwa ajili ya watoto hao ambayo itatumika kuwapatia ujuzi na elimu mbalimbali kama kilimo ili hata wazazi wanao watuma kuomba hela wakose wa kuwatuma.

No comments:

Powered by Blogger.