LIVE STREAM ADS

Header Ads

Programu mpya za kuinufaisha jamii kuanza kutolewa wilayani Misungwi

Wasiliana na BMG Blog/ BMG Online TV kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misunwgi (Misungwi CDTTI) kinatarajia kuanza kutoa programu mpya za muda mfupi kwa wanafunzi wake, lengo likiwa kuwanufaisha wanajamii.

Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dongo Nzori Dongo (pichani) aliyasema hayo jana kwenye Mahafali ya Nane ya Chuo hicho (Tazama Hapa) ambapo kwa sasa kinatoa mafunzo katika ngazi za Cheti cha Msingi (Basic Technician Certificate), Cheti (Technician Certificate) na Stashahada (Ordinary Diploma) kwa kuratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu la Ufundi (NACTE) chini ya mfumo wa “NTA Levels”.

Aidha itakumbukwa kwamba chuo hicho kilianzishwa mwaka 1982 Mlale mkoani Ruvuma na mwaka 1983 kilihamishiwa Misungwi mkoani Mwanza na kuanza kutoa mafunzo ya Cheti cha Msingi cha Maendeleo ya Jamii Ufundi (Basic Certificate Course in Civil Engineering-BCC) na ilipofika mwaka 2008 kilibadilishwa Mitaala na kuanza Program za Uhandisi, Ujenzi na Maendeleo ya Jamii. Tazama BMG Online TV hapa chini
Mahafali ya nane ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi yafana

No comments:

Powered by Blogger.