LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kampuni ya Acacia yawaandaa watanzania kuwa viongozi bora

Wasiliana na BMG Blog/ BMG Online TV kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kampuni ya uchimbaji madini Acacia imeendelea kuwajengea uwezo wafanyakazi wake lengo likiwa ni kuwaandaa kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika kampuni hiyo pamoja na kutekeleza vyema majukumu yao ndani na nje ya kampuni.

Meneja Mkuu Uboreshaji Tija wa kampuni hiyo inayomiliki migodi ya Acacia North Mara, Buzwagi na Bulyanhulu, Janet Reuben Lekashingo aliyasema hayo jana Jijini Mwanza, kwenye mahafali ya sita ya wafanyakazi 93 waliohitimu mafunzo maalum ya uongozi (Rainbow Leadership Development Programme).

Katika kipindi cha miezi sita, wahitimu wamemaliza kozi nane tofauti za uongozi zikiwemo ufanisi katika mawasiliano, utamaduni wa uongozi, ustawi mahala pa kazi, kanuni za tahadhari za kampuni na malalamiko, kusimamia mahusiano ya kibinafsi, kujenga imani na kutumia mifumo ya ndani ambapo hadi kufikia mwaka jana, asilimia 96 ya wafanyakazi wa Acacia ni watanzania.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.