LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wafanyakazi wa kigeni wapungua katika kampuni ya Acacia

Wasiliana na BMG Blog/ BMG Online TV kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.

Annastanzia Mbunda ambaye ni mmoja wa wafanyakazi wa Acacia waliohitimu mafunzo maalum ya uongozi akizungumza na wanahabari katika hafla/ mahafali yaliyofanyika jana Malaika Hotel Jijini Mwanza.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Programu za mafunzo mbalimbali zinazoendeshwa na kampuni ya Acacia kwa wafanyakazi wake wazawa, zimewezesha kampuni hiyo kupunguza utegemezi wa wafanyakazi wa kigeni kwa asilimia 85 katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Meneja Mkuu Uboreshaji Tija wa kampuni ya Acacia, Janet Reuben Lekashingo aliyasema hayo jana Jijini Mwanza, wakati akizungumza kwenye Mahafali ya sita ya wafanyakazi 93 wa kampuni hiyo waliohitimu mafunzo maalum ya uongozi (Rainbow Leadership Development Programme) na kuongeza kwamba hadi kufikia mwaka jana, asilimia 96 ya wafanyakazi wa Acacia walikuwa watanzania. Tazama BMG Online TV hapa chini
Kampuni ya Acacia yawaandaa watanzania kuwa viongozi bora

No comments:

Powered by Blogger.