BAKWATA mkoani Geita kuanza utekelezaji wa miradi mikubwa
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Joel Maduka, Geita
Baraza Kuu
la Waislamu (BAKWATA) mkoani Geita linatarajia kuanza ujenzi wa jengo la
ghorofa nne litakalogharimu zaidi ya shilingi biloni tatu ambapo litakuwa na
Msikiti, maduka zaidi ya 100, kumbi za mikutani pamoja na vyumba vya kulala
wageni.
Mwenyekiti
wa Baraza hilo, Alhaji Said Karidushi amesema kuanzishwa kwa miradi hiyo
kutafungua mwanya mkubwa wa kuwasaidia watu mbalimbali hususani katika sekta ya
elimu na afya.
Karidushi
amesema pia Baraza hilo linatarajia kujenga Chuo cha Mafunzo kitakachowahudumia
wanajamii kutoka dini zote.
Naye Sheikh
Mkuu wa Mkoa Geita, Alhad Yusuf Kabaju
amesema miradi hiyo inatarajiwa kuanza mwaka huu na kukamilika kwa wakati kwani
lengo ni kuhakikisha BAKWATA inakua kiuchumi na kutimiza malengo yake.
No comments: