Wanahabari wahimizwa kushiriki kwenye hatua za utungaji sheria
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwezeshaji, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza kwenye mafunzo ya siku mbili kuanzia jana kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu yenye lengo la kuwajengea uwezo kuhusu sheria mpya za habari. Mafunzo hayo yanafanyika Mjini Bariadi yakiandandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika MISA tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Internews ofisi ya Tanzania.
“Lengo la
mafunzo haya ni kubadilishana uzoefu, kukumbushana kwamba kuna sheria za vyombo
vya habari, upatikanaji wake ulikuwaje, zinatunufaisha kwa kiwango gani na zina
vikwazo gani kwetu wanahabari”. Alisisitiza Sengiyumva Gasirigwa ambaye ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo na kuongeza;
“Waandishi
wa habari mnao wajibu wa kushiriki kwenye michakato ya upatikanaji wa sheria za
vyombo vya habari kuanzia kwenye
utungaji wake na hata maboresho ya sheria hizo pamoja na kanuni zake
ikizingatiwa kwamba michakato hiyo ni endelevu”.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mshiriki, Aidan Mhando akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki Dinna Maningo akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mshiriki mwenzao, Dinna Maningo wakati akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
"Energizing session"
“Kipindi cha
uchaguzi ni kipindi muhimu sana kwetu wanahabari ambapo tunahitaji kufanya kazi
kwa ushirikiano na watoa taarifa wetu hivyo mafunzo haya yatawaongeza kiwango
cha uelewa kuhusu sheria za vyombo vya habari ikiwemo Sheria ya Haki ya Kupata
Taarifa ya mwaka 2016 ili kuboresha utendaji kazi wenu katika chaguzi zijazo”. Sengiyumva
Gasirigwa, Mwezeshaji mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mara,
Mwanza na Simiyu yaliyoandaliwa na MISA Tanzania kwa kushirikiana na Internews.
“Waandishi
wa habari tunao wajibu wa kushiriki kwenye michakato ya upatikanaji wa sheria
za vyombo vya habari kuanzia kwenye
utungaji wake na hata maboresho ya sheria hizo pamoja na kanuni zake
ikizingatiwa kwamba michakato hiyo ni endelevu”. Sengiyumva Gasirigwa, Mwezeshaji mafunzo kwa
waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mara, Mwanza na Simiyu yaliyoandaliwa na
MISA Tanzania kwa kushirikiana na Internews.
Tazama BMG Online TV haoa chini
No comments: