LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jaji ataka wabunge kutunga sheria rafiki "ahimiza Kiswahili mahakamani"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe. Sam Rumanyika (pichani) amehimiza muhimiri wa bunge kuhakikisha unatunga sheria rafiki na zinazoeleweka kwa wananchi, hatua itakayosaidia upatikanaji wa haki.

Mhe. Jaji Rumanyika ameyasema hayo leo, kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria nchini yaliyoanza Januari 31, 2019 ikiwa ni mwaka wa 23 tangu maadhimisho hayo yaasisiwe mwaka 1993 na mwaka wa nne tangu maboresho ya madhimisho hayo yaanze kufanyika mwaka 2015 ambapo elimu kwa umma hutolewa kwa njia mbalimbali ikiwemo maonesho.

Aidha Mhe. Jaji Rumanyika amesema angetamani kuona lugha ya Kiswahili ikitumika mahakamani katika kuendesha kesi na mashauri mbalimbali huku akiwahimiza wadau muhimu wa sheria wakiwemo waandishi wa habari, kufanya kazi kwa welezi ili kuhakikisha haki inapatikana kwa 
 Kaimu Sheikh Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke akitoa dua kabla ya kuanza maadhimisho ya Siku ya Sheria katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
 Kaimu Sheikh Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke akitoa dua kabla ya kuanza maadhimisho ya Siku ya Sheria katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
 Baba Askofu kanisa Anglikana, Godfrey Mbelwa akisoma sala kabla ya kuanza maadhimisho ya Siku ya Sheria katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
 Kiongozi wa dhehebu la Bohora akitoa dua kabla ya kuanza maadhimisho ya siku ya sheria katika viunga vya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
 Mawakili wa kujitegemea na Serikali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Mawakili mbalimbali.
 Viongozi wa serikali na dini wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Gwaride kwenye maadhimisho hayo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.