LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Waziri Mazingira akagua chanzo cha maji Mto Luegu mkoani Ruvuma

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Sima akisalimiana na viongozi wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma baada ya kuwasili wilayani hapo kwa lengo la kubaini changamoto za kimazingira na kuweka mikakati ya kuhifadhi Ikolojia ya Vyanzo vya Maji.
Na Lulu Mussa
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Sima akitoka kukagua chanzo cha maji cha Mto Luegu kilichopo katika Kijiji cha Ngwinde, Kata ya Litola Wilaya ya Namtumbo. Chanzo mto Luegu kinachangia asilimia 19 ya maji katika Mto Rufiji. Katika ziara yake wilayani Namtumbo, Naibu Waziri Sima amesisitiza uhifadhi endelevu katika eneo hilo ili chanzo hicho kisivamiwe kwa shughuli za kibinadamu. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Sima akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme vitambulisho maalum vya wakaguzi wa mazingira vilivyotolewa na ofisi yake kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004. Vitambulisho hivyo maalum vitawezesha wakaguzi wa mazingira kutekeleza majukumu yao kiufanisi ikiwa ni pamoja na kusimamia uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira.

No comments:

Powered by Blogger.