LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yahimizwa kuchukua madeni ya TANESCO

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Busega, Dkt. Raphael Chegeni (kushoto), akizungumza jana wakati wa majumuisho ya ziara ya Kamati yake iliyolenga kutembelea mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme wa gesi asilia Kinyerezi I (Kinyerezi I Extension) jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati hiyo wakipatiwa maelezo ya utekelezaji wa mradi huo.
Wajumbe wa Kamati hiyo wakipatiwa maelezo ya utekelezaji wa mradi huo.
Mjumbe wa Kamati, Charles Mwijage akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Mbunge wa Kasulu Vijijini, Vuma Augustine.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Mhandisi Dkt. Alexander Kyaruzi (aliyesimama), akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati, Dkt. Raphael Chegeni na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka akizungumza kwenye ziara hiyo.
Dkt. Mwinuka akimkaribisha Mbunge wa Karatu, Willy Qambalo huku Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi Dkt. Kyaruzi akishuhudia, wakati wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), ilipofanya ziara kwenye kituo cha kuzalisha umeme wa gesi asilia Kinyerezi I.

NA K-VIS BLOG /Khalfan Said
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, imeridhishwa na mabadiliko makubwa ya kiutendaji ndani ya Shirika la Umeme Nchini TANESCO, ambapo ndani ya kipindi kifupi limeondokana na utegemezi wa ruzuku ya serikali na sasa linajiendesha lenyewe. 

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Raphael M. Chegeni wakati wa hitimisho la ziara ya Kamati kwenye mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme utokanao na gesi asilia, Kinyerezi 1 (Kinyerezi I Extension) jijini Dar es Salaam.

"TANESCO ni Shirika ambalo limekumbwa na changamoto nyingi miaka ya nyuma, lakini tumefurahi kuona kwamba baadhi ya mambo yaliyokuwa mazito sana mmefanikiwa kuyatatua na hii ni dalili njema ni nzuri sana kwa sababu sasa hata serikali yetu ya awamu ya tano toka imeingia madarakani, TANESCO badala ya kuwa mtegemezi mkuu wa ruzuku ya serikali, hivi sasa Shirika halitegemei tena ruzuku ya serikali hili ni jambo jema sana". Alisema na kuongeza;

"Mmetoka kwenye ruzuku na sasa mnakua mnajitegemea haya ni mafanikio endeleeni kupunguza gharama, na mpanue wigo wa watumiaji wa umeme, watanzania wanahitaji umeme wenye gharama nafuu na haya ndio malengo ya serikali ya awamu ya tano". Alisema Dkt. Chegeni.

Alisema mpango wa Serikali wa kujenga umeme wa maji Rufiji ni mpango sahihi kabisa na watanzania wote wazalendo lazima waunge mkono juhudi hizo kwa sababu unahitajika umeme ambao ni wa gharama ya chini ili umfikie kila mtanzania.

Aidha Mwenyekiti huyo aliahidi kuwa Kamati yake itaiomba serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina iangalie namna gani madeni yanayoikabiri TANESCO kwa miaka mingi yanaondolewa ili iweze kujiendesha kikamilifu na kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka alisema Shirika limejiwekea mikakati endelevu ili kuhakikisha linaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ambapo baada ya kudhibiti deni ambalo Shirika limekuwa likidaiwa kwa muda mrefu, sasa wameanza kuwalipa wadai wa Shirika sambamba na kuondokana na kutegemea ruzuku ya kutoka serikalini.

Aidha Mkurugenzi wa Uwekezaji kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Lightnes Mauki alisema kwa sasa TANESCO imeanza kulipa madeni na tangu mwezi wa Februari mwaka huu 2019 wamelipa bilioni 38.7.

No comments:

Powered by Blogger.