LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ilivyokuwa mapokezi ya mwili wa mama mzazi wa Vicky Kamata

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto) ameungana na ndugu, jamaa na marafiki kuupokea mwili wa Paulina Kasama Selemani ambaye ni mama mzazi wa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa Geita, Vicky Kamata (kulia) katika uwanja wa ndege wa Mwanza ukitokea Jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Geita kwa ajili ya taratibu zaidi za mazishi. Mama Paulina Kasama Selemani pia alikuwa dada wa Mkuu wa Mkoa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.
#BMGHabari
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Mkuu wa Mkoa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo kufuatia kifo cha dada yake Mama Paulina Kasama Selemani. Wengine ni wanafamilia pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) kwenye mapokezi ya mwili wa dada yake, mama Paulina Kasama Selemani. Kulia ni mtoto wa marehemu ambaye pia ni mbunge wa viti maalum (CCM) mkoani Geita, Vicky Kamata.
Tazama BMG Online TV hapa chini 

No comments:

Powered by Blogger.