LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mahakama mkoani Mwanza yawahukumu wafanyabiashara wa madini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa Mwanza imewahukumu kwa pamoja wafanyabiashara wanne wa madini Jijini Mwanza kifungo cha miaka 60 jela (kila mmoja miaka 15) ama kulipa faini shilingi milioni 529.8 (wote), baada ya kukiri makosa tisa yaliyokuwa yanawakabili ikiwemo uhujumu uchumi, rushwa na utakatishaji fedha. Ni baada ya mahakama hiyo kupewa haki kisheria kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 1/ 2019.

Watuhumiwa wengine wanane ambao walikuwa askari polisi wamerudishwa rumande hadi Aprili 10, 2019 baada ya kukana mashtaka yanayowakabili. Waliohukumiwa ni Hassan Sadiq, Emmanuel Mtemi, Kisabo Nkinda pamoja na Sajid Hassan ambapo walikuwa wakitetewa na Mawakili Emmanuel Safari na Michael Nasimile.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Mkoa Mwanza, Mhe. Rhoda Ngimilanga. Washtakiwa walikamatwa Januari 04,2019 wakituhumiwa kutorosha shehena ya madini ya dhahau, kukutwa na mamilioni ya fedha huku askari wakidaiwa kupewa rushwa ili kuwasindikiza.
#PamojaDaimaBMG

No comments:

Powered by Blogger.