LIVE STREAM ADS

Header Ads

Benki ABC yachangia huduma za maendeleo wilayani Kilindi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwakilishi wa benki ABC, Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akikabidhi msaada wa mabati kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo.
Mwakilishi wa benki ABC, Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja na Asmah Abubakar (kushoto) kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi msaada wa mabati kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo (kulia).
Mwakilishi wa benki ABC, Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja na Asmah Abubakar (kushoto) kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi msaada wa mabati kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo (kulia).
Sauda Salum Mtondoo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilindi akikabidhi mabati yaliyotolewa na BancAbc kwa walimu wa shule ambazo zimenufaika na msaada huo.
Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja na Asmah Abubakar kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi msaada wa mabati kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo
Mwakilishi wa benki ABC, Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akipeana mkono na Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo baada ya kukabidhi msaada wa mabati 200. Wengine katika picha ni Asmah Abubakar na Raphael Kalinga kutoka BancAbc.

Na Ahmad Michuzi
BancABC kupitia huduma yetu ya Mkopo Rahisi imejidhatiti kuweza kuhakikisha kwamba inaendeleza mazingira ya elimu katika wilaya ambazo benki hiyo inafanya shughuli zake kupitia miradi yake ya kusaidia jamii.

Sisi BancABC inaamini kwenye umuhimu wa elimu bora katika jamii hapa Tanzania na kwa hivyo inaunga mkono Serikali ya awamu ya tano katika miradi mbalimbali ya elimu kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu na kuweza kuifikia kila jamii na hasa maeneo ya vijijini kwa wale ambao wako kwenye hali duni.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi, Emmanuel Nzutu ambaye ni mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi alisema; "Kwa kuunga mkono juhudi za serikali za kutoa elimu bure kwa kila Mtanzania kuanzia chekechekea hadi kidato cha nne, leo Bancabc tunatoa msaada wa mabati 200 kwa wilaya ya Kilindi, na msaada huu tunaukabidhi hapa kwa Mkuu wa Wilaya, Sauda Salum Mtondoo".

Tunatoa wito kwa wateja wetu na wale ambao pia sio wateja wetu kujiunga na Bancabc na kuchangamkia huduma mbalimbali ikiwemo mikopo yenye riba nafuu.

No comments:

Powered by Blogger.