Header Ads

Waliokamatwa na dhahabu wahukumiwa miaka 60/ askari bado

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Biswalo Mganga amefafanua mwenendo wa kesi ya uhujumu uchumi nambari 1/2019 inayowahusisha wafanyabiashara wanne wa madini pamoja na askari polisi wanane waliokamatwa na dhahabu kilo 323.6 yenye thamani ya shilingi bilioni 27.018 pamoja na fedha shilingi milioni 305 kati ya Januari 04 na 05 mwaka huu.

Itakumbukwa jana Machi 27, 2019 washtakiwa wanne ambao ni wafanyabiashara wa madini walihukumiwa na mali zao kutaifishwa baada ya kukiri makosa dhidi yao huku washtakiwa wengine wanane waliokuwa askari polisi wakirejeshwa rumande baada ya kukana mashtaka ambapo kesi yao itasikilizwa Aprili 10, 2019.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.