LIVE STREAM ADS

Header Ads

Taasisi ya MISA Tanzania yatoa mafunzo kwa Watumishi wa Mahakama Kanda ya Moshi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
BMG Habari
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afya (MISA) tawi la Tanzania kupitia ufadhili wa taasisi ya FESI Media Africa, imeandaa mafunzo ya siku tatu kuanzia leo Machi 14, 2019 kwa Watumishi wa Mahakama Kanda ya Moshi.

Mafunzo hayo yaliyowashirikisha Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo, Watunza Kumbukumbu, Makatibu Muhtasi, Walinzi pamoja na Wahudumu wa Mapokezi mahakamani yamelenga kuwajengea uwezo kuhusu namna ya kuboresha huduma kwa wateja na haki ya kupata taarifa.

Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Jaji Mfawidhi, Mhe. Patricia Fikirini amesema yatasaidia kuleta mabadiliko makubwa katika utoaji wa huduma na taarifa kutoka idara mbalimbali za Mahakama.

Naye Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Salome Kitomary alisema pamoja na mambo mengine, pia washiriki wa mafunzo hayo watajifunza jinsi ya kutoa taarifa na kuomba taarifa, ujuzi wa misingi na sifa za kushughulikia malalamiko, manufaa ya kushughulikia malalamiko kwa wakati, jinsi ya kuwahudumia wateja.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya MISA tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa amebainisha kwamba mafunzo hayo ni mwendelezo wa mpango wa muda mrefu kati ya taasisi hiyo na muhimili wa Mahakama katika kuboresha huduma kwa wateja pamoja na utoaji wa taarifa kwa wakati.
Kaimu Mkurugenzi MISA Tanzania, Sengiyumvya Gasirigwa akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Kaimu Mkurugenzi MISA Tanzania, Sengiyumvya Gasirigwa akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Salome Kitomari akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Wajumbe wakifuatilia mafunzo hayo.
Mgeni rasmi, Kaimu Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Mhe. Patricia Fikirini akifungua mafunzo hayo.
Washiriki wakimsikiliza mgeni rasmi wakati akifungua mafunzo hayo.
Mwezeshaji, Wakili James Malenga pamoja na washiriki wengine wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Picha ya pamoja.
Mwenyekiti wa Misa Tanzania, Salome Kitomari (kulia), akisalimiana na mgeni rasmi Kaimu Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Mhe. Patricia Fikirini

No comments:

Powered by Blogger.