LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wakazi wa Misungwi kuondokana na kero ya maji

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Antony Sanga (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) kuhusu utekelezaji wa mradi wa maji katika Mji wa Misungwi uliopo katika Kijiji cha Nyahiti wilayani humo. Kulia ni Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa.
Mraji wa maji Nyahiti-Misungwi unatarajiwa kuondoa adha ya upatikanaji wa maji safi na salama wilayani Misungwi.
Sehemu ya mashine za kusukuma maji kwenye chanzo cha maji Nyahiti wilayani Misungwi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto) akipongezwa na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (katikati), baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa mradi wa maji Nyahiti-Misungwi. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mwanza, Dkt. Antony Diallo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wakazi wa Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, wanatarajia kuondokana na adha ya upatikanaji wa maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mradi wa maji uliopo katika Kijiji cha Nyahiti wilayani humo.

Mradi huo ambao uko kwenye hatua za mwisho kukamilika, jana uliwekewa jiwe la msingi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambapo hadi kukamilika kwake utagharimu shilingi bilioni 12.85 ikiwa ni fedha za Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB), Shirika la Maendeleo la Ufarasa (AFP) pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mradi huo unatekelezwa na kampuni ya “China Civil Engeneering Construction Corparation” chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) ikiwa kupitia mpango wa uboreshaji huduma za maji safi na usafi wa mazingira ya Ziwa Victoria.
Tazama hapa chini BMG Online TV

No comments:

Powered by Blogger.