LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mama asimulia tukio la mtoto wake kufanyiwa ukatili wa kingono

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na Asha Shaban, Mara
March 13 ilikuwa siku ya maumivu makali yasiyo futika akilini kwa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne (jina linahifadhiwa), anayesadikiwa kubakwa akiwa shuleni katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara, tukio hili bado limeacha watu wengi wakiwa vinywa wazi.

Mama mzazi wa mtoto huyo, Mariamu Adam anasema siku ya tukio alimpokea mtoto wake kama kawaida akitokea shule na walipoanza safari ya kurudi nyumbani kutoka anaposhushwa mtoto na gari la shule, mtoto alianza kulalamika kuwa anaumia anomba ambebe.

Anasema alichukua jukumu la kumbeba mtoto wake mpaka nyumbani ambapo kama kawaida alisema anaporudi kutoka shule humuandalia chochote kitu ili mtoto apate kunywa lakini wakati anampa chakula, mtoto alirudia tena kumwambia kuwa anaumia.

"Mama njoo unione nimeumia huku, nilipigwa na butwaa nikijiuliza amekuwaje ndipo nilipo chukua jukumu la kumpeleka kituo cha polisi". Amesema Adam.

Anasema baada ya kufika kituo cha polisi alipewa fomu namba tatu (Pf3) na kumpeleka mtoto huyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mara.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mara, Joachim Iyembe amekiri kumpokea mtoto huyo Machi 13, 2019 majira ya saaa nane usiku huku mtoto akiwa na hali mbaya hususani maumivu kwenye sehemu za siri.

Ameongeza kuwa majibu ya awali yanaonyesha kuwa ni kweli mtoto amekutwa hana bikira jambo ambalo linaonyesha yawezekana alikuwa anazoeshwa kuingiliwa mara kwa mara bila ya kupata maumivu.

Amesema ni kweli siku hiyo walipo mpokea mtoto alikuwa ana uvimbe katika sehemu zake za siri huku ikionyesha aliingiliwa kinguvu na kusababisha mtoto huyo kupata uvimbe na kuchanika katika sehemu za siri.

Iyembe anasema kuwa uchunguzi bado unaendelea kwakuwa wanasubiria majibu ya vipimo ambayo ndio yatatoa majibu kamili kama mtoto huyo aliingiliwa na binaadamu ama alipata madhara hayo kwa njia nyingine ambapo alisema kuwa wameisha chukua sampuli za "DNA" ambazo zitalinganishwa na baadhi ya watuhumiwa ambao wamekamtwa mpaka hivi sasa.

Kamanda wa Polisi Mkoa Mara, Juma Ndaki ameahidi kuzungumzia tukio hilo baada ya uchunguzi kukamilika. "Bado tunaendelea na uchunguzi wa taarifa hii na pale uchunguzi utakapo kamilika tutawajulisheni hivyo kwa sasa sina taarifa kamili". Alisema Ndaki.

No comments:

Powered by Blogger.