LIVE STREAM ADS

Header Ads

Watuhumiwa wa utakatishaji fedha wafikishwa mahakamani mkoani Mara

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na Asha Shaban, Mara
Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamalaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mara (MUWASA), Hawaiju Gantala amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za utakatishaji fedha kwenye maradi wa maji katika Wilaya Bunda mkoani humo.

Jana Gantala pamoja na wenzake wawili alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa Mara na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa Mara wakishtakiwa kwa makosa sita ya kuisababishia Serikali hasara wakati wa utekelezaji wa mradi wa maji mwaka 2011 wilayani Bunda.

Watuhumiwa wengine waliofikishwa mahakamini Kaimu Mkutugenzi wa Maji, Emanuel Ruyobya na Mkurugenzi wa kampuni ya Nyakirang’anyi Construction Company Limited, Mauza Nyakiranganyi.

Awali akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake, Naibu Kamanda wa Takukuru Mkoa Mara, Daniel Kapakala alisema taasisi yake imekamilisha uchunguzi kwa watuhumiwa hao huku wengine wawili uchunguzi ukiendelea ili nao wafikishwe mahakamani.

Mkuu wa Mashitaka Mkoa Mara, Valence Mayenga alisema kesi inayo wakabili watuhumiwa hao ni kesi namba 2/2019 ya kutakatisha fedha kiasi cha shilingi bilioni 9.13 za ujenzi wa mradi wa maji katika Wilaya Bunda.

Mayenga alisema washitakiwa hao walitenda kosa kinyume na kifungu cha 306 cha sheria cha kanuni ya adhabu ambapo kwa pamoja walisababishia mamlaka upotevu wa shilingi milioni 613 ambapo katika shitaka la pili linamuhusu Mkurugenzi wa MUWASA akidaiwa kwamba mwaka 2017 alitengeneza hati ya uongo ya kumaliza mradi wa maji huo wa maji.

Gantala alifanya hivyo huku akijua kuwa Mkandarasi Mahuza Nyakirang’anyi hakuwa amemaliza kazi hati hiyo ililenga kuihujumu mamaka kiasi cha shilingi milioni 7.5 huku kosa la tatu linalomkabili Mkurugenzi huyo likiwa ni kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri wake kinyume na kifungu cha 22 cha sheria ya kuzuai na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Shitaka la nne linalowakabili watuhumiwa wote watatu ambao ni Mkurugenzi wa MUWASA Hawaiju Gantala, Maunza Nyakirang’anyi na Emanueli Ruyobya ni kutakatisha fedha kiasi cha shilingi milioni sita kinyume na kifungu cha sheria 12 (d) na 13 (a ) cha sheria ya kuzuia utakatishaji fedha namba 12 mwaka 2006.

Shitaka la tano linalowakabili washitakiwa wote watano ni kuisababishia MUWASA hasara ya fedha kiasi cha shilingi milioni 205 na kosa la sita linawakabili washitakiwa wote ni kosa la kusababishia MUWASA hasara ya fedha kiasi cha shilingi milioni 325.

Hakimu Raimu Mushi alisema washitakiwa hao hawatakiwi kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kusilikiza kesi ya uhujumu uchumu na kuwataka washitakiwa hao kwenda rumande mpaka pale kesi itakapo tajwa alipokea maombi ya pande zote mbili kutoka upande wa mashitaka na upande wa utezi ambapo waliridhia kutajwa tena kwa kesi hiyo tarehe Aprili 03, 2019.

Kufuatia mashtaka hayo hakimu Rahim Mushi aliagiza upande wa mashtaka kuwaleta mahakamani hapo washtakiwa wengine wawili ambao ni Mhandisi wa MUWASA, Peter Kisobari pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya Forteles, Juvenali Sherianga ambaye pia alikuwa akitekeleza mradi huo ambao hadi sasa haujakamilika.

Mradi huo wa maji ambao ulikuwa utekelezwe kwa kipindi cha mwaka mmoja umekuwa ukisuasua hali iyopelekea viongozi mbalimbali wa Serikali Kuu akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutoa maagizo kwa TAKUKURU kufanya uchunguzi juu ya watu waliotuhumiwa kukwamisha utekelezaji wa mradi huo.

Mwaka jana akiwa ziarani mkoani Mara, Rais Dkt. Magufuli aliagiza mamlaka zinazohusika kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika na kuagiza hatua kali kuchukuliwa dhidi ya watakaobainika kuukwamisha.

Rais Dkt. Magufuli alitengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentine Mlolowa baada ya kupata taarifa kuwa alishindwa kuchukua hatua baada ya kupewa taarifa ya uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU Mkoa Mara kufuatia maagizo ya Waziri Mkuu, Kassimm Majaliwa.

No comments:

Powered by Blogger.