LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi wahimizwa kutunza mifumo ya majitaka

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkurugenzi wa Usimamizi Huduma za Majitaka wa Jijini Dar es salaam (DAWASA), Shabani Mkwanywe (kulia) akizungumza na wanahabari katika Wiki ya Maji Duniani iliyoanza Machi 16 hadi 22, 2019 ambapo DAWASA inaadhimisha kwa kusikiliza kero za wananchi katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Mkurugenzi wa Usimamizi Huduma za Majitaka wa DAWASA, Shabani Mkwanywe (kushoto) akieleza machache mbele ya wanahabari juu ya mifumo ya Maji Taka.
Watoa huduma wakiendelea kutoa elimu na kutatua kero za wananchi waliofika katika Wiki ya Maji Duniani.

Wananchi wakisoma vipeperushi.

Na Cathbert Kajuna, Kajunason/ MMG
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es Salaam (DAWASA) inatarajia kujenga miradi 50 ya jamii ya kuchakata majitaka katika maeneo yasiyopangwa ili kutatua changamoto za unyonyaji maji ikiwemo kuzuia magonjwa ya mlipuko. 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Usimamizi Huduma za Majitaka, Shabani Mkwanywe alisema miradi hiyo ya jamii itajengwa katika maeneo ambayo huwa inakumbwa na magonjwa ya mlipuko. Alisema pia kutajengwa vituo 25 vya kusafirishia Majitaka kwa maeneo ambayo hayawezi kufikiwa kirahisi. 

"Miradi hii itawasaidia kujibu changamoto za wakazi asilimia 70 kwa wanaotumia vyoo vya shimo na asilimia 20 vyoo vya matenki". Alisema Mkwanywe. 

DAWASA inabuni miradi hiyo ikiwa wanasubiri kuanza kwa miradi mikubwa mitatu ambayo ni ile wa Jangwani, Kurasini na Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam. 

Alisema Changamoto kubwa inayowakabili ni mifumo mingi ya majitaka ilijengwa miaka 50 na 70 na Dar es Salaam haikuwa na watu wengi kama ulivyokwa sasa. Wananchi wanatupa TakaNgumu na kusababisha kuziba. 

Aliongeza kuwa ili kukabiliana na wananchi kukosa huduma ya majitaka, DAWASA wamejipanga kununua malori ili kuweza kusaidia wananchi kupita mtaani na kukusanya kwa bei watakayoweza kuimudu tofauti na sasa huduma hiyo imekuwa ikitolewa na watu binafsi kwa gharama ya juu.

No comments:

Powered by Blogger.