LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wakulima waanza kunufaika na Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasha trekta aina ya Ursus katika zoezi fupi la kukabidhi matrekta 16 yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.8 kwa baadhi ya Wenyeviti wa Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) mkoani Mwanza kwenye hafla ya ufunguzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Kongani ya Kanda ya Ziwa.

Matrekta hayo yanakopeshwa kwa wakulima kupitia vyama vya ushirika ikiwa ni ushirikiano baina ya benki hiyo na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Bodi ya Pamba Tanzania na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania ambapo hafla hiyo ilifanyika Machi 19, 2019 Jijini Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto) akimkabidhi ufunguo Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Ugata kilichopo wilayani Magu, Enock Ng'ombe (kulia). Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa trekta Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Ushirika Mgundama, Getrude John kwenye hafla hiyo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.