LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Mkuu kufungua soko la dhahabu mjini Geita

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majawaliwa jumapili Machi 17, 2019 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye zoezi la ufunguzi wa soko la dhahabu Mjini Geita.

Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Robert Gabriel amesema pamoja na soko hilo, pia kutakuwa na jumla ya vituo vinane vya uuzaji dhahabu ambavyo ni Lwamgasa, Nyarugusu, Katoro, Bwanga, Chato Mjini, Ushirombo, Masumbwe na Msalala.

Mkoa Geita umekuwa wa kwanza kuanzisha vituo/ soko ya dhahabu hapa nchini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli kwa Wizara ya Madini kusimamia uanzishwaji wake ili kuziba mianya ya uuzaji madini kiholela hali inayochochea utoroshaji madini na hivyo kuikosesha serikali mapato. 
Na Joel Maduka, Geita
Tazama BMG Online TV haoa chini

No comments:

Powered by Blogger.