LIVE STREAM ADS

Header Ads

Marufuku kutoa mikopo kiduchu kwa wajasiriamali- Waziri

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati) amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuacha tabia ya kutoa mikopo kiduchu kwa vikundi vya wajasiriamali kupitia fedha za asilimia 10 kama ilivyo takwa la kisheria.

Waziri Mwalimu aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, ambayo kwa ngazi ya Mkoa Mwanza yalifanyika katika uwanja wa Kisesa wilani Magu, Machi 08, 2019.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati) akiwa na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Anders Sjoberg pamoja na viongozi mbalimbali kwenye maadhimisho ya Wanawake Duniani ngazi ya Mkoa Mwanza
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani huwadhimishwa kila mwaka Machi 08 lengo likiwa ni kutambua mchango wa mwanamke katika maendeleo na kuhamasisha kupinga hadharani vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Katika Maadhimisho hayo, Waziri Ummy Mwalimu alizindua kampeni ya kitaifa iitwayo SAWA (Shetta Against Women Abuse) ambapo msanii Shetta atatumia ushawishi wake kufikisha ujumbe kwa jamii kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto, kampeni hiyo inaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Msanii Shetta akitumbuiza kwenye maadhimisho hayo.
Burudani kutoka kwa Shetta ambapo alitambulisha wimbo wake unaohamasisha jamii kuachana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake.
Kutoka kushoto ni Balozi wa Sweden nchini Tanzania Anders Sjoberg, Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa UN Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa shirika la UN Women Hodan Addou wakifurahia jambo kwenye maadhimisho hayo.
Kampeni ya Shetta Against Women Abuse (SAWA) itatumia muziki kwa kushirikiana na wasanii mbalimbali, wadau wa maendeleo pamoja na wananchi katika kubadili fikra ili kuleta usawa wa kijinsia katika jamii.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.