LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali kuja na Sheria kali ya kupambana na mimba na ndoa za utotoni

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Mgeni rasmi, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza kwenye Maadhimisho ya Wanawake Duniani katika uwanja wa Kisesa, Wilaya Magu mkoani Mwanza, Machi 08, 2019.

Waziri Mwalimu alisema Serikali inakuja na Sheria ya kupambana na mimba na ndoa za utotoni ambapo atakayemuoa ama kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya msingi ama sekondari atahukumiwa miaka 30 gerezani. Sheria hiyo pia inaeleza kwamba hata mshenga na wahudhuriaji/ wale wala ubwabwa pia watasukumwa ndani wakikutwa wamehudhuria ndoa ya mwananafunzi
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi akitoa salamu kwenye maadhimisho hayo.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Anders Sjoberg akitoa salamu zake kwenye maadhimisho hayo.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, linaloshughulikia masuala ya wanawake UN Women, Hodan Addou akitoa salamu zake kwenye maadhimisho hayo.
Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez akitoa salamu kwenye maadhimisho hayo.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa kila mwaka Machi 08 ili kutambua mchango wa mwanamke katika kuchochea maendeleo pamoja na kuhamasisha jamii kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Maandamano ya wanawake kutoka Kituo cha Polisi Kisesa kuelekea kwenye uwanja wa Kisesa wilayani Magu.
Mashirika mbalimbali ikiwemo Shirika la Kutetea Haki za Wasichana na Wanawake KIVULINI la Jijini Mwanza yalishiriki kwenye maadhimisho hayo kwa kuandaa mabanda yaliyotumika kutoa elimu kuhusu masuala ya kuondokana na ukatili wa kijinsia.
Kauli mbinu ya Siku ya  Wanawake Duniani 2019 ni "Badili Fikra, Kufikia Usawa wa Kijinsia, Kwa Maendeleo Endelevu".
Kikundi cha Sungu Sungu Misungwi kikitumbuiza ngoma ya kisukuma kwenye maadhimisho hayo
Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya Magu Dkt. Philemon Sengati,  Balozi wa Sweden nchini Tanzania Anders Sjoberg, Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa UN Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa shirika la UN Women Hodan Addou wakifurahia jambo kwenye maadhimisho hayo.
Katika Maadhimisho hayo, Waziri Ummy Mwalimu alizindua kampeni ya kitaifa iitwayo SAWA (Shetta Against Women Abuse) ambapo msanii Shetta atatumia ushawishi wake kufikisha ujumbe kwa jamii kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto, kampeni hiyo inaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Kampeni ya Shetta Against Women Abuse (SAWA) itatumia muziki kwa kushirikiana na wasanii mbalimbali, wadau wa maendeleo pamoja na wananchi katika kubadili fikra ili kuleta usawa wa kijinsia katika jamii.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.