Header Ads

Rais Magufuli awatunuku wachezaji Taifa Stars

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametoa ahadi ya kuwapa viwanja wachezaji pamoja na viongozi wa timu ya Taifa, Taifa Stars katika Jiji la Dodoma, baada ya timu hiyo kufanikiwa kufuzu michuano ya AFCON 2019 kwa kuifunga Uganda 3-0 jana. 

Pia ametoa ahadi kwa timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Total AFCON 2019 inayotarajiwa kufanyika nchini.

 Aidha Rais Dkt. Magufuli ametoa ahadi kiwanja kwa bondia Hassan Mwakinyo baada ya kuibuka na ushindi wa TKO dhidi ya bondia Gonzalez kutoka Algentina.

Rais Magufuli ametoa ahadi hizo leo kwenye hafla ya kuwapongeza wachezaji wa Taifa Stars na bondia Mwakinyo Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo pia amejumuika nao kwenye chakula cha mchana.
VideoCredit: TBC
#PamojaDaimaBMG

No comments:

Powered by Blogger.