LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanafunzi mkoani Njombe kunufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Taasisi ya Evolution of Youth Ability Organization (Evo Refto) imetoa fursa ya ufadhili wa masomo (Scholarship) kwa wanafunzi waotarajia kuhitimu kidato cha sita mwaka huu 2019 ambapo ufadhili huo utahusisha masomo katika ngazi ya Shahada ya kwanza (Bachelor Degree) nchini India.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Elimu na Vijana wa shirika hilo, Athumani Fue imeeleza kwamba ufadhili huo utawalenga wahitimuwa wanne watakaofanya vizuri kwenye mtihani wa kidato cha sita mwaka huu katika kozi za Sayansi na Afya.

“Tutatoa nafasi nne kwa Mkoa Njombe ambapo kila Wilaya itapata nafasi moja katika Wilaya zote ambazo ni Njombe, Ludewa, Makete pamoja na Wanging’ombe”. Alisema Fue.

Alisema mbali na ufadhili huo, pia shirika hilo litatoa nafasi 15 za ufadhili wa asilimia 50 kwa wanafunzi wa Mkoa Njombe watakaofanya vizuri kwenye mtihani wao wa kidato cha sita mwaka huu.

“Tunatarajia kufanya ziara maalum mkoani Njombe kuanzia Aprili 05 hadi 10, 2019 ili kuzungumza na wanafunzi wa kidato cha sita na kuwahamasisha kusoma kwa bidii ili kunufaika na fursa hii”. Alifafanua Fue.

Aidha Fue aliongeza kwamba kwamba fursa hiyo imetokana na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya taasisi ya Evolution of Youth Ability Organization (Evo Refto) na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Njombe, Neema Mgaya (CCM) ambaye amekuwa akijitahidi kuboresha mazingira ya elimu mkoani humo kwa kushiriki na kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa, mabweni pamoja na upatikanaji wa vitabu katika shule mbalimbali.

#PamojaDaimaBMG

No comments:

Powered by Blogger.