LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wadau mkoani Geita waketi kujadili mikakati ya kupambana na Ukatili

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Meneja wa shirika la kimataifa la kutetea haki za watoto, Plan International mkoani geita, Marcely Madubi akizungumza wakati wa kikao cha kujadili mikakati shirikishi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani humo.
Baadhi wa washiriki wa kikao wakifuatilia kikao hicho.
Meneja Mradi wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Watoto na Wanawake kutoka shirika la Plan International, Emma Mashobe akizungumzia mikakati ya kupambana na changamoto ya ukatili mkoani humo.

Na Joel Maduka, Geita
Imebainika bado watoto wa kike wameendelea kukumbana na changamoto nyingi katika jitihada za kufikia ndoto zao za kimaisha ikiwani pamoja na kukosekana kwa fursa ya kusoma kutokana na kuwepo kwa vitendo vya ubaguzi wa kijinsia, uelewa na uwezo mdogo wa wazazi na walezi, mimba za utotoni ambazo ni tatizo kubwa hasa ndani ya mkoa wa Geita ambapo kwa kipindi cha mwaka jana zaidi ya mimba 300 zimelipotiwa kutokea.

Hayo yalibainishwa na Meneja wa shirika lisilo la kiserikali la Plan Internationall,  Marcely Madubi wakati akitoa taarifa ya vitendo vya ukatili kwenye kikao cha wadau wa kujadili mikakati shirikishi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Alphendo Mjini Geita.

Alisema mkoa wa Geita bado umeendelea kukubwa na tatizo kubwa la kuwepo kwa mimba za utotoni ambazo zimekuwa zikichochea kwa kiasi kikubwa wanafunzi wa kike kushindwa kufikia malengo ambayo wamejiwekea na sababu kubwa ikionyesha ni kuwepo kwa uwezi duni kwa baadhi ya familia na wengine wazazi wao na walezi kushindwa kuwa karibu kwaajili ya kuwapa malezi ambayo ni bora kwani wengi wao wamekuwa wakiwaachaniza wanafunzi wa kike kuishi kwa kupanga vyumba kutokana na kuwepo kwa umbali wa shule.

"Watoto wengi ambao tumeshawai kuzungumza nao na kuona mazingira wanayotoka wengi wao wanasema ni ugumu wa maisha ya familia ndio chanzo kikubwa kinacho wapelekea kujikuta wakiingia kwenye mahusiano na mwisho wa siku kupatiwa ujauzito mfano Geita watoto mia tatu na kumi na tano kwa mwaka jana wameshabebeshwa ujauzito hii ni hatari sanaa kwa maisha ya watoto wetu". Alisema Madubi.

Akimwakilisha mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Elikana Haruni alitumia nafasi hiyo kuwasihii viongozi wa dini kutoa elimu juu ya vitendo vya ukatili kwa waumini wao.

"Tunaamini viongozi wa dini wakisisimama kwa pamoja na serikali kutoa elimu juu ya vitendo hivi vya ukatili watakuwa wamesaidia kwa nafasi kubwa kupunguza matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza mala kwa mala na kusababisha kuwanyima haki wanawake na watoto". Alisema Elikana.

Christopher Mushi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alisema bado kunatizo kubwa la vitendo vya ukatili kwa wanandoa kutokana na kwa kila wanawake mia moja ambao wameolewa wanawake 35 wamefanyiwa ukatili wa kimwili huku 36 wakifanyiwa ukatili wa kiakili na wenza wao.

Aidha baadhi ya washiriki wa kikao hicho wametoa mchango wao juu ya vitendo vya ukatili ambavyo vimeendelea kufanyika kwenye jamii juu ya nafasi ya mwanamke kwenye masuala ya kurithi.

"Tunatambua mwanamke ananafasi kubwa ya kurithi mali kutoka kwa mzazi au hata mume lakini suala hili bado kuna tatizo kubwa sanaa kwa baadhi ya jamii basi tuombe serikali kupitia wizara waendelee kutoa elimu hili kuwasaidia wakina mama na watoto wa kike". Alisema Mzee Othuman Chatanga.

No comments:

Powered by Blogger.