LIVE STREAM ADS

Header Ads

CRDB yashiriki kongamano la AIESEC katika Chuo cha SAUT Jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Taasisi ya AIESEC inasifika kwa mchango wake mkubwa wa kutengeneza vijana ili kuwa viongozi bora na mahiri duniani kwa miaka ijayo. Nchini Tanzania pia taasisi hiyo inafanya kazi kwa kuwakutanisha vijana wenye ndoto ya kuwa viongozi bora hapo baadae ambapo pia inatoa fursa kwa vijana kujiunga.

Machi 23, 2019 taasisi hiyo imeandaa kongamano katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT tawi la Malimbe Jijini Mwanza, kuhusu masuala ya uongozi na namna ya kufikia maendeleo endelevu ya Milenia na kuwashirikisha wanafunzi wa chuo hicho pamoja na viongozi mbalimbali.

Wawakilishi wa benki ya CRDB pia walishiriki kongamano hilo ikizingatiwa kwamba benki hiyo ni mshirika mkubwa wa taasisi ya AIESEC ambapo imekuwa ikifadhili shughuli zake mbalimbali.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Meneja Biashara kutoka benki ya CRDB Tawi la Mwanza, Dkt. Danford Muyango (PhD) akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo.
Afisa Rasilimali Watu- Mafunzo kutoka benki ya CRDB Makao Makuu Jijini Dar es salaam, Emmanuel Tesha akizungumza kwenye kongamano hilo.
Washiriki wa mdahalo huo wakimsikiliza Afisa Rasilimali Watu- Mafunzo kutoka benki ya CRDB Makao Makuu Jijini Dar es salaam, Emmanuel Tesha wakati akichangia mada.
Afisa Mauzo kutoka benki ya CRDB, Gerolida Samwel akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo. Alitumia fursa hiyo pia kuelezea huduma ya Sim Banking inayotolewa na benki ya CRDB.
Msimamizi wa Biashara kutoka benki ya CRDB, Evalyne Minzani akichangia mada kwenye kongamano hilo.
Rais wa taasisi ya AIESEC nchini Tanzania, Yvette Tackie (kulia), akiongoza mada kwenye kongamano hilo.
Rais wa taasisi ya AIESEC nchini Tanzania, Yvette Tackie (kulia), akizungumza kwenye kongamano hilo.
Baadhi ya wanachama wa AIESEC kutoka nchi mbalimbali duniani wakijitambulisha.
Kufurahia huduma ya Sim Banking kutoka CRDB, piga nambari *150*03# 
Washiriki wakifuatilia kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Picha ya pamoja baada ya kongamano.
Picha ya pamoja.
Meneja Biashara kutoka benki ya CRDB tawi la Mwanza, Dkt. Daniford Muyango (kulia), akiteta jambo na mmoja wa wanachama wa AIESEC kutoka nchini Mondovia.
Meneja Biashara kutoka benki ya CRDB tawi la Mwanza, Dkt. Daniford Muyango (kushoto), akiwa kwenye picha ya pamoja na Ris wa taasisi ya AIESEC nchini Tanzania, Yvette Tackie (kulia), baada ya kutamatika kongamano hilo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.