Wadau Tanzania wakutana kutathmini juhudi za ukombozi wa mwanamke
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Sehemu ya washiriki wa warsha ya siku moja iliyolenga kutathimini mustakabali wa juhudi za ukombozi wa mwanamke nchini kuelekea miaka 25 ya mkutano wa Beijing hapo mwakani.
Mwenyekiti wa TGNP, Mama Assen Muro akitoa rai kwa wadau wote kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa changamoto zilizopo ili wanawake waweze kupiga hatua katika kufikia maendeleo endelevu.
Mwenyekiti wa TGNP Mtandao, Mama Assen Muro akimueleza jambo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Stella Ikupa alipowasili kwenye warsha hiyo.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Stella Ikupa akizungumza na washiriki wa warsha hiyo ambapo aliwahimiza kutorudi nyuma katika jitihada za kutetea haki na nafasi ya mwanamke katika jamii.






Washiriki wakifuatilia kwa karibu mawasilisho.
Mdau wa masuala ya wanawake ambaye pia ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Rachel Chibwete akiwasilisha majibu kwa niaba ya kundi lililojumuisha wabunge, madiwani pamoja na waandishi wa habari.
Wanafunzi kutoka shule ya Sekondari Manchali iliyopo Chamwino Jijini Dodoma.

Washiriki wakishikana mikono kama ishara ya umoja na mshikamano ambayo kwa pamoja waliafiki kuwa ni nguzo muhimu katika kufanikiwa kuitetea nafasi ya mwanamke katika jamii.
Sehemu ya washiriki wakipata picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Stella Ikupa

Na Fredy Njenje
Ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kilele ni tarehe 8 ya mwezi Machi kila mwaka,wadau mbali mbali wamekutana jijini Dodoma kujadili na kutathimini mustakabali wa juhudi za ukombozi wa mwanamke nchini kuelekea miaka 25 ya mkutano wa Beijing hapo mwakani.
Warsha hiyo siku moja ambao iliyowakutanisha washiriki zaidi ya 100 kutoka kote nchini wakiwemo wadau mbalimbali likiwajumuisha wanawake wakiwakilisha makundi mbalimbali, wabunge, madiwani, wanasheria, waandishi wa habari pamoja na wanafunzi wa vyuo na sekondari, iliandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na TAWLA, Landesa, Msichana Initiative, Haki Ardhi, Haki Elimu, Care International na TAMWA.
Mkutano huo wa Beijing uliofanyika mwaka 1995 ulilenga kuwashirikisha na kuwawezesha wanawake katika maendeleo ili kuimarisha mapambano dhidi ya umaskini na hiyo yote ni kwa wanawake kushiriki katika shughuli za kimaendeleo.
Katika kuhakikisha kila mshiriki anachangia mawazo,ilitumika njia ya kuwagawa katika makundi na kujadili maana, uelewa, umuhimu, mitizamo pamoja na changamoto la azimio la Beijing katika jamii na nchi kiujumla ambapo miongoni mwa hoja zilizoibuliwa katika kuboresha jitihada za kuleta usawa wa kijinsia ni pamoja na elimu juu ya azimio bado inahitajika sambamba na ushirikishwaji wa jamii yote kwa ujumla sambamba na kueleza faida ya usawa wa kijinsia kuanzia ngazi ya familia ili kutengeneza kizazi chenye kuelewa manufaa yake.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanasimamiwa na kauli mbiu inayosema “Badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu”.
No comments: