LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanawake wahimizwa kuchukia rushwa ya ngono

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani akionyesha bidhaa zinazozalishwa na kikundi cha wanawake wilayani Ileje.
BMG Habari
Maafisa kutoka katika Dawati la Jinsia Wilayani Ileje wakiandamana katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, jana Machi 08.

Wanawake Mkoani Songwe wameaswa kutonyamazia vitendo vya rushwa ya ngono ili waweze kujikomboa kifikra, kiuchumi na kisiasa katika harakati za kufikia usawa wa kijinsia kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Akisoma jana hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brig Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa wilayani Ileje, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo alisema rushwa ya ngono inapaswa ithibitiwe kwa nguvu zote

“Nawasihi sana wanawake wanaokumbana na udhalilishaji huu wa kuombwa rushwa ya ngono watoe taarifa katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) pia wananchi wengine watoe taarifa mara tu wanapokutana na matatizo ya rushwa ili taasisi husika ziweze kushughulikia”, alisema Palingo

Ameongeza kwa kuziagiza halmashauri za Mkoa wa Songwe kuhakikisha zinaendelea kupiga vita unayanyasi na ukatili wa kijinsia, taasisi zote zinazohusika na mapambano hayo ikiwa ni pamoja na dawati la jinsia kuwachukulia hatua wote wanaofanya vitendo hivyo.

Palingo alieelekeza kuwa halmashauri ziweke mazingira mazuri ya masoko ya bidhaa na mazao yanayozalishwa na wanawake, kutenga fedha kwaajili ya kuwawezesha wanawake kuwa na uwezo wa kumiliki viwanda na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake.

Akisoma risala kwa niaba ya wanawake, Afisa Maendeleo ya Jamii, Roida Kyomo amlisema wanawake wamekuwa wakizalisha kidogo kutokana na ukosefu wa masoko, elimu na mitaji wakti uwezo wa kuzalisha bidhaa na mazao mengi wanayo.

Kyomo aliongeza kuwa uwepo wa mashauri 442 ya unyanyasaji wa kijinsia unaonyesha kuwa tatizo hilo bado lipo hivyo ameiomba serikali kuendelea kuhamasisha jamii kuachana na mila kandamizi kwa wanawake ili muda unaotumika katika kusuluhisha matatizo hayo utumike katika kuzalisha mali ili kukuza uchumi.

No comments:

Powered by Blogger.