LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Meya Manispaa ya Iringa atembelea kiwanda cha "Dustless Smart Chalk"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa, Joseph Lyata alipotembelea kiwanda cha chaki cha "Dustless Smart Chalk".
Baadhi ya chaki zinazotengenezwa kiwandani hapo.

Na Fredy Mgunda, Iringa
Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa, Joseph Lyata ameagiza shule zote katika Manispaa hiyo kutonunua chaki kutoka nje ya kiwanda Dustless Smart Chalk kwa kuwa kiwanda hicho kinatengeneza chaki zilizo bora na zinazofaa.

Lyata amesema kiwanda cha chaki kilichopo Manispaa ya Iringa kinatengeneza chaki zilizo na kiwango bora cha kutumiwa na walimu wakati wa kufundisha ili kuinua uchumi wa kiwanda hicho.

"Tusipowaunga mkono vijana na kiwanda hiki cha kutengeneza chaki tutakuwa tunaua uchumi wa wananchi wa Manispaa ya Iringa hivyo lazima walimu watumie chaki zinazotengenezwa kiwandami hapa". Alisema Lyata alipotembelea kiwandani hapo.

Mmoja wa wanakikundi wa kiwanda cha Dustless Smart Chalk, Prisca Masalanga amesema kinakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa za vifaa bora vya kuzalishia bidhaa hii ya chaki. Masalanga alisema changamoto kubwa ambayo wanakumbana nao ni kukosa soko la kudumu.

No comments:

Powered by Blogger.