Zoezi la ukaguzi wa vyoo bora lapamba moto Kaya kwa Kaya wilayani Ilemela
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Judith Ferdinand, BMG
Wakazi
wilayani Ilemela wamehimizwa kubadili fikra na kuwa na utamaduni wa kujenga
vyoo bora na kuvitumia badala ya kusubiri hadi mamlaka za Serikali ziwafikishe
kwenye vyombo vya sheria.
Afisa Afya
wilayani humo, Petro Joseph ametoa rai hiyo wakati akizungumzia zoezi la
ukaguzi wa vyoo bora katika ngazi ya Kaya, lililoanza mwezi Januari mwaka huu
ambalo hufanyika kila baada ya miezi mitatu.
“Wananchi
wawe na tabia ya kujenga na kutumia vyoo bora, wasisubiri hadi wafikishwe
kwenye vyombo vya sheria”. Alisema Joseph.
Alibainisha
kwamba Sheria ya Afya ya Jamii namba moja ya Mwaka 2009 inatoa mwongozo wa
kuwafikisha mahakamani wananchi wasio na vyoo bora hivyo wananchi wasisubiri
hatua hiyo badala yake wawe na vyoo bora hatua itakayosaidia kuoambana na
maginjwa ya milipuko.
#PamojaDaimaBMG
No comments: