LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mfuko wa WCF wang'ara kitaifa jijini Mbeya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama akimkabidhi Masha Mshomba ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) tuzo na cheti . Mfuko wa WCF umekuwa mshindi katika masuala ya afya na usalama kazini baina ya taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Tuzo hiyo imetolewa katika Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani Aprili 30, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama akimkabidhi Cheti cha ushiriki wa Siku ya Afya na Usalama Duniani Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulssalaam Omary jijini Mbeya.
Tuzo na cheti katika masuala ya afya na usalama kazini baina ya Taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.  Tuzo hiyo imetolewa katika Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (kushoto) akipata maelezo ya Mfuko kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulssalaam Omary (wa pili kulia) alipotembelea banda hilo. Wa tatu kushoto ni Mwakilishi wa ILO Afrika, Jealous Chirove na Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Anthony Mavunde (katikati kulia).
Mkurugenzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Masha Mshomba (katikati) akifurahia pamoja na wafanyakazi wa baada ya Mfuko kuwa Mshindi katika masuala ya afya na usalama kazini baina ya Taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Masha Mshomba (wa pili kushoto) pamoja na wafanyakazi wengine wa WCF baada ya kupata Tuzo na Cheti cha ushindi wa huduma bora za Bima.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wakifurahia baada ya kuibuka mshindi katika masuala ya afya na usalama kazini baina ya Taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu Wenye Ulemavu), Stella Ikupa (aliyeketi) akipata maelezo ya mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kutoka kwa Mkurugenzi wa huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulssalaam Omary (wa pili kulia) walipo tembelea banda hilo.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulssalaam Omary akimpa maelekezo Dkt. Kiva Mvungi kutoka Geita Gold Mine kuhusiana na viwango vya ulemavu kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.
Afisa Matekelezo Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Amina Likungwala akitoa zawadi kwa wadau mbali mbali waliotembelea banda la WCF.
Wadau mbalimbali waliotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wakipata maelezo juu ya mafao na shughuli za mfuko huo.
Afisa afya na usalama mahali pa kazi kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Robert Duguza akitoa maelezo juu ya huduma na mafao yatolewayo na mfuko huo.
Watu mbalimbali wakiendelea kutembela katika banda la mfuko wa WCF.
Afisa Mwandamizi, Afya na Usalama Mahali pa Kazi kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Tumaini Kyando akitoa maelezo ya mafao yanayotolewa na WCF.
Meneja Tathmini, Vihatarishi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Naanjela Msangi akifafanua umuhimu wa kufanya tathimini ya vihatarishi katika maeneo ya kazi.
Afisa Mwandamizi wa Mahusiano kwa Umma kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Sebera Fulgence akimkabidhi kava la gurudumu mdau aliyetembelea banda la WCF.
Afisa Matekelezo Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Amina Likungwala akitoa zawadi kwa wadau mbalimbali waliotembelea banda la WCF.
Baadhi wa watumishi wa mfuko wa WCF.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza mbele ya banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi WCF wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Duniani 2019 yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya.

No comments:

Powered by Blogger.