LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Kasesela ashiriki mkesha wa wanafunzi Chuo Kikuu cha Iringa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akiongea na wanafunzi na viongozi wa Chuo Kikuu cha Iringa waliokuwa kwenye mkesha wa kuabudu na kuomba ambapo aliwahimiza kujiandaa kabla hawajaanza kusali ili kuweza kuyafikisha maombi yao vilivyo kwa Mwenyezi Mungu.
Mkuu wa Wilaya Iringa, Richard Kasesela akiwa kwenye picha ya pamoja na moja ya kwaya iliyotoa burudani kwenye mkesha huo.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuku cha Iringa wakiwa kwenye mkesha huo.

Na Fredy Mgunda, Iringa
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amewataka waamini wote kujiandaa kabla hawajaanza kusali ili kuweza kuyafikisha maombi yao vilivyo kwa Mwenyezi Mungu.

Akizunguza wakatika wa mkesha na kuabudu ulioandaliwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa, Kasesela alisema kila jambo ambalo unatarajia kulifanya ni lazima ujiandae kwanza.

"Mimi katika maisha yangu kabla sijafanya jambo huwa natafuta muda wa kulifikiria jambo hilo ndio nalifanyia kazi ndio maana mara nyingi nimekuwa na maamuzi sahihi katika kufanya kazi zangu kila wakati". Alisema Kasesela.

Kasesela aliwataka wanafunzi hao kufanya maombi ya kukiombea chuo hicho ili kuendelea kuwa chuo bora hapa nchini na nje ya nchi na kuendelea kuutangaza mkoa wa Iringa kwa kuwa jina la chuo hicho limebeba jina la mkoa wa Iringa.

Chuo hiki kilitaka kufungwa kwa ajili ya mambo ambayo hayana miguu wa kichwa hivyo naowaomba mkiombee chuo hiki ili kisije kikafungwa au kufikiriwa kufungwa tena maana kimekuwa kikitoa elimu iliyo bora sana” alisema Kasesela.

Aidh Kasesela alisema kwanini kanisa la KKKT limekuwa kanisa ambalo limegawanyika katika kanda mbalimbali ambapo kila ukanda unafanya mambo bila kuwa na ushirikiano wowote ule na dayosisi nyingine.

Kasesela alisema kuwa mgawanyiko huo utasabisha vyou vingi vya KKKT kufa kutokana na kutokuwa na ushirikiano kama ilivyokuwa na vyuo vingine hapa.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gavile aliwataka wanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa kukesha na kukiombea chuo hicho mara kwa mara.

"Ombeni nanyi mtapewa kwa kuwa mnaomna kwa nia njemba na mungu nimoto ambao unaweza kuwabariki kila mmoja wetu hapa hivyo nawaomba tena kuendelea kuomba". Alisema Askofu Gavile.

No comments:

Powered by Blogger.