LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la KIVULINI latafiti changamoto zinazowakabili wanawake wajasiriamali

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Shirika la Kutetea Haki za Wasichana na Wanawake KIVULINI la Jijini Mwanza kwa kupitia ufadhili wa taasisi ya Maendeleo Jumuishi I4ID, limekutana na makundi mbalimbali yanayowawakilisha wanawake wajasiriamali/ wafanyabiashara wadogo kutoka Halmashauri za Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza ili kubainisha changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya biashara na namna ya kuzitatua.

Kikao hicho kilifanyika jana ikiwa ni sehemu ya utafiti unaofanywa na shirika la KIVULINI kwa kushirikiana na taasisi ya I4ID pamoja na Halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela ili kupata mikakati kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa pamoja wa kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wadogo hususani wanawake na walemavu.

Wakizungumza kwenye kikao hicho, Annastazia Wambura na Hidaya Juma ambao ni baadhi ya wafanyabiashara wadogo Jijini Mwanza walieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili ambazo wangependa zitafutiwe ufumbuzi kuwa ni pamoja na ukosefu wa elimu ya biashara inayojumuisha mitaji, mikopo, masoko pamoja na maeneo rafiki ya kufanyia biashara.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema utafiti wa awali unaonyesha kwamba wanawake wengi wanaingia kwenye ujasiriamali baada ya kukabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo mimba kabla ya wakati, migogoro ya ndoa kuvunjika, kutelekezwa ama kunyang'anywa mirathi hivyo kufahamu changamoto zinazowakabili kibiashara itasaidia kuboresha mazingira yao kwa ajili ya ustawi wao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye kikao hicho ambapo alibainisha kwamba utekelezaji wa mpango wa pamoja wa kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wadogo katika Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza utawasaidia wafanyabiashara hao kujitambua na hususani kuwa na nidhani ya masuala ya fedha tofauti na ilivyo sasa ambapo baadhi yao wamekuwa wakikopa kwenye taasisi moja kulipa mikopo kwenye taasisi nyingine.
Mwakilishi kutoka taasisi ya I4ID akizungumza kwenye kikao kazi hicho.
Mmoja wa washiriki wa kikao hicho akiwasilisha mikakati iliyotolewa na washiriki kupitia makundi yao.
Mmoja wa wafanyabiashara wadogo Jijini Mwanza, Annastazia Wambura akiwasilisha mikakati iliyotolewa na washiriki kwenye makundi.
Mshiriki wa kikao hicho akiwasilisha mapendekezo yaliyotolewa na washiriki wengine kupitia makundi.
Dr. Nandera Mhando ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (Mtafiti), akifafanua jambo kwenye kikao hicho.
Washiriki wa kikao hicho wakifuatilia mada.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Mwanza, Isaac Ndasa akitoa neno la shukrani kwenye tamati ya kikao hicho ambapo alilishukru shirika la KIVULINI kupitia ufadhili wa taasisi ya I4ID kwa kuja na mkakati wa kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wadogo hususani wanawake na walemavu.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.