LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la KIVULINI lahimizwa kuanzisha programu zake wilayani Chato

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Chato mkoani Geita, Eliurd Mwaiteleke amesisitiza umuhimu wa Shirika la Kutetea Haki za Wasichana na Wanawake (KIVULINI) la jijini Mwanza, kuanzisha programu zake katika Halmashauri hiyo ili kusaidia utoaji wa elimu ya ukatili katika jamii.

Ameyasema hayo leo Mei 30, 2019 jijini Mwanza katika warsha ya kuweka mikakati ya kuboresha huduma rafiki kwa wahanga wa ukatili na vijana ikiwa ni sehemu ya utekelezaji mradi wa “sauti yangu katika kupunguza mimba katika umri mdogo Manispaa ya Ilemela” unaosimamiwa na Shirika la KIVULINI.

Mwaitekeleke alikuwa akitoa uzoefu na mafanikio yaliyopatikana katika Halmashauri ya Misungwi kupitia utekelezaji wa mpango mkakati wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya watoto na wanawake (MTAKUWWA) kabla ya kuhamishiwa Halmashauri ya Chato Agosti 13, 2018.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kushoto) akitoa ahadi ya Shirika hilo kuanzisha programu za kuzuia ukatili wa kijinsia mkoani Geita. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato, Eliurd Mwaiteleke.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.