Header Ads

Timu za Tanzania zaingia kambini kujinoa na mashindano ya Castle Africa 2019

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na Mwandishi Maalum, Dar
Timu "Four Ways Park FC" yenye makazi yake Kinondoni jijini Dar es Salaam na "Girls Queens" yenye makazi yake Msimbazi Kariakoo jijini Dar es Salaam zimeingia kambini rasmi kujiandaa na mashindano ya Castle Africa 5s (5 aside) yanayotarajia kuanza kutimua vumvi Juni 7 na 8, 2019 katika uwanja wa Taifa wa zamani (Shamba la Bibi) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Balozi wa Castle Lager Africa nchini Tanzania, Ivo Mapunda alisema timu zote ziko vizuri tayari kwa kuwakilisha Watanzania katika fainali za Kimataifa na ushindi ni lazima kulingana na maandalizi waliyonayo na watakayoendelea nayo.

Mwaka huu Tanzania tutawakilishwa na timu ya wanaume kutoka Four Ways ya Kinondoni na timu ya wanawake ya Girls Queens kutoka Msimbazi Kariakoo kwa ujumla timu zote ziko sawa na ziko tayari kwa fainali hizo na leo rasmi sasa wanaingia kambini kwa kujiandaa na fainali hizo.

Nae Meneja wa bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli alizitaji nchi shiriki zinazotarajiwa kushiriki mashindano hayo ya Africa 5s kuwa ni Africa Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Lethoto, Uganda, wenyeji Tanzania na nchi alikwa ya Nigeria.

Kikuli alisema nchi hizo zikiwakilishwa na timu ya wanaume na wanawake zinatarajiwa kuwasili nchini Juni 5,2019 tayari kwa fainali za Castle Africa 5s.
Juni 6, 2019 timu zitakabidhiwa vifaa vya michezo katika Hoteli ya Lamada jijini Dar es Saalaam tayari kwa kuanza mashindano rasmi Juni 7 na 8, 2019.

Alisema "tunawaomba watanzania wapenda michezo wajitokeze kuja kuzishangilia timu zao zinazowakilisha nchi katika Fainali hizo za Castle Africa 5s".

Mwisho Kikuli alisema fainali hizo zinatarajiwa kuhudhuria na Balozi wa Castle Africa 5s, Samwel Eto’o hivyo tujitokeze kwa wingi kuja kumshuhudia mchezaji mkongwe wa Zamani pamoja na kupiga nae picha.

wameibuka mabingwa katika Bonanza kubwa la Soka lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Posta Kijitonyama kwa udhamini wa kampuni ya Bib nchini (TBL) kupitia bia yake ya Castle Lager na hivyo kuzawadiwa kikombe, medali za dhahabu, fedha taslimu shilingi 1,500,000/=, caton ya bia ya Castle Lager pamoja na kuwakilisha nchi katika fainali za Caslte Africa 5s zinazotarajiwa kufanyika mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Four Ways Park Fc waliutwaa ubingwa kwa point saba wakifuatiwa na Jacks Pub FC kwa pont nne ambao walizawadiwa medali za silva, catoni ya bia ya Castle Lager na pesa taslimu shilingi 900,000/=.
Mshindi wa tatu ni katika fainali hizo ni Meeda Night Club FC ambao walipata pointi tatu na hivyo kuzawadiwa medali fedha, caton ya bia ya Castle Lager pamoja na pesa taslimu shilingi 600,000/=

Akizungumza na wachezaji, waandishi wa habari pamoja na wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye bonanza hilo, Menager bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli alianza kwa kuwapongeza mabingwa Four Ways Park Fc kwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ikiwa ni mara ya pili sasa kufanyika kwa Tanzania na akawaomba zawadi walizopata zikawe chachu ya maandalizi bora ya fainali za Castle Afica 5s ambazo zinatarajiwa kufanyika nchini Tanzania.

Kikuli pia aliwapongeza timu ya pili na ya tatu kwa ushindi na akato pongezi kwa timu shiriki zote kwa kujitoa kwao katika fainali hizo na kwa jinsi hiyo wakajiandae kwa mashindano mengine mwakani.

Pamela aliutaja mchakato ulivyokuwa wa kuzipata timu ambao ulianzia kwenye baa 60 za jijini Dar es Salaam ambapo baa zilishindana kwa kununua bia za Castle Lager na kukusanya vizipo na mwisho tukapata timu 32 zilizoongoza na ndizo zimeweza kushiriki bonanza mpaka kumpata bingwa ambaye ni Four Ways Park FC.

Nae Balozi wa bia ya Castle Africa 5s Tanzania, Ivo Mapunda aliishukuru kampuni ya bia nchini (TBL) kwa uratibu mzuri wa mashindano ya Castle Africa 5s mwaka huu kwani yamekuwa na hamasa ya hali ya juu na kuwaomba waendelee kudhamini mashindano hayo kwani kupitia bonanza hili wapo waliopata marafiki na mambo mengine mengi kwa sababu ya bonanza hili kupitia bia ya Castle Lager ambayo imetuunganisha pamoja.

No comments:

Powered by Blogger.