LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwenge wa Uhuru 2019 wahitimisha mbio zake mkoani Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Umati mkubwa wa wananchi pamoja na viongozi mbalimbali waliojitokeza Mei 14, 2019 kuupokea Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Mwawile kilichopo Kata ya Nhundulu Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, ukitokea mkoani Shinyanga.

Mwenge huo unakabidhiwa leo Mei 22, 2019 mkoani Simiyu baada ya kukimbizwa nchi kavu kilomita 855.11 na majini notiko maili 72 katika Mkoa Mwanza ukipitia miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 15.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wakazi wa Kata ya Ibinza wilayani Misungwi wakiwa katika eneo la mradi wa maji ya bomba Ibinza ambapo hata hivyo Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali aligoma kuzindua mradi huo uliogharimu shilingi milioni saba ikiwa ni fedha za Halmashauri baada ya kukosekana taarifa ya vipimo vya ubora wa maji hayo yanayotoka katika chanzo cha maji KASHWASA.
Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Shukrani Tungaraza (kulia) akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa mradi wa maji ya bomba Ibinza kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Mzee Mkongea Ali (wa pili kushoto) pamoja na timu yake.
Mwenge wa Uhuru uliweka jiwe la msingi la ufunguzi wa nyumba moja ya waalimu inayochukua watumishi sita (six in one) katika Shule ya Sekondari Isakamawe wilayani Misungwi iliyogharimu shilingi milioni 141 ikiwa ni fedha za serikali kupitia mfuko wa elimu.
Nyumba ya watumishi katika Shule ya Sekondari Isakamawe wilayani Misungwi.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda akitoa shukrani zake baada ya Mwenge wa Uhuru kuweka jiwe la msingi la ufunguzi wa nyumba wa waalimu katika Shule ya Sekondari Isakamawe.
Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali pia aligoma kuweka jiwe la msingi kwenye matengenezo ya barabara ya Misungwi-Mondo kwa kiwango cha moramu yenye ulefu wa kilomita 23 iliyogharimu shilingi milioni 425.9 baada ya kukosekana kwa baadhi ya taarifa ikiwemo vipimo vya ubora wa ndondo kwa ajili ya ujenzi wa makaravati/ madaraja.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali pamoja na timu yake wakipima uimara wa barabara ya Misungwi-Mondo ambapo hata hivyo aligoma kuweka jiwe la msingi kwenye barabara hiyo baada ya kukosekana baadhi ya taarifa.
Mhandisi wa TARURA wilayani Misungwi, Elzabron Kayungi (kulia) akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Misungwi-Mondo kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali (kushoto).
Mwenge wa Uhuru 2019 ulifungua jengo la kitengo cha bima ya afya NHIF katika hospitali ya Wilaya Misungwi.
Mwonekano wa jengo la bima ya afya NHIF katika hospitali ya Wilaya Misungwi.
Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Misungwi (kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu ujenzi wa jengo la kitengo cha bima ya afya NHIF katika hospitali ya Wilaya Misungwi kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019 (katikati).
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali akikata upete kuashiria uzinduzi wa jengo la kitengo cha bima ya afya katika hospitali ya Wilaya Misungwi.
Uzinduzi wa jengo la kitengo cha bima ya afya katika hospitali ya Wilaya Misungwi.
Kiongozi wa mbio za Mwnge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali pia alizindua kampeni ya Ziro Malaria- Inaanza na Mimi wilayani Misungwi.
Kiongozi wa mbio za Mwnge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali pamoja na timu yake akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi mbalimbali wa hospitali ya wilaya Misungwi.
Mwenge wa Uhuru 2019 pia ulizindua Klabu ya wapinga rushwa katika Shule ya Msingi Misungwi.
Mwenge wa Uhuru 2019 ulizindua kiwanda cha vijana wajasiriamali katika Kata ya Usagara wilayani Misungwi kinachotengeneza mikanda ya "Gypsum".
Mwenyekiti wa kikundi cha kutengeneza Gypsum Usagara wilayani Misungwi, Salum Haji akitoa taarifa ya mradi huo.
Kiongozi wa mbio za Mwnge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali (katikati) akitoa pongezi kwa kikundi cha vijana wajasiriamali Usagara kwa kubuni mradi huo wa utengenezaji mikanda ya Gypsum na kuagiza Halmashauri ya Misungwi kuendelea kuwawezesha kupitia mikopo ya vijana ili kukuza mradi huo.
Kiongozi wa mbio za Mwnge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali (kushoto) akimpongeza Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda (katikati) kwa kusimamia vyema miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.
Mwenge wa Uhuru 2019 ulikagua uendelevu wa mradi wa kutengeneza gesi ya majumbani wa "Mwanza Gaz" na kuridhishwa na mradi huo.
Taarifa kuhusu kiwanda cha gesi ya majumbani "Mwanza Gaz" kilichopo wilayani Misungwi.
Mwenge wa Uhuru 2019 ulipowasili katika kiwanda cha kutengeneza gesi ya majumbani "Mwanza Gaz" katika eneo la Usagara wilayani Misungwi.
Kiongozi wa mbio za Mwnge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali (kushoto) pamoja na timu yake akiwapongeza viongozi wa kiwanda cha gesi ya majumbani "Mwanza Gaz" baada ya kukuta kinaendelea vyema na uzalishaji.
Mwenge wa Uhuru 2019 ulipowasili katika kiwanda cha gesi ya majumbani "Mwanza Gaz" katika eneo la Usagara wilayani Misungwi.
Kiongozi wa mbio za Mwnge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali pamoja na timu yake wakijionea namna mitungi inavyojazwa gesi kwa ajili ya matumizi.
Kiongozi wa mbio za Mwnge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali akiwapongeza viongozi wa kiwanda cha kuzalisha gesi ya majumbani "Mwanza Gaz" kwa uendelevu wa kiwanda hicho.
Viongozi mbalimbali wakitoka katika eneo la kiwanda cha kuzalisha gesi ya majumbali "Mwanza Gas" kilichopo Usagara wilayani Misungwi.

No comments:

Powered by Blogger.