Wadau wakutana kujadili utata wa Sheria za Vyombo vya Habari
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva akichangia mada katika warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari.


Wadau mbalimbali wa habari wakiwa kwenye warsha hiyo.





Katika kuendeleza hamasa na kutetea uhuru wa kujieleza katika jamii, taasisi ya MISA Tanzania na shirika la utetezi wa sheria na haki za kijamii la ICNL imewakutanisha wadau mbalimbali katika warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari.
Warsha hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya habari, asasi za utetezi wa haki za binadamu, wanasheria pamoja na wahadhiri wa vyuo vikuu ikifanyikia mjini Bagamoyo ikilenga kujadili namna sheria za vyombo vya habari zinavyo athiri mazingira ya kazi za kiuandishi pamoja na uhuru wa kujieleza.
Akielezea umuhimu wa uwepo wa sheria rafiki katika kufanya mazingira yawe salama kwa tasnia ya habari, Aloys Habimana kutoka shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL lenye makao makuu yake nchini Marekani alisema changamoto ya sheria zisizo rafiki kwa taaluma ya habari na uhuru wa kujieleza ni changamoto sehemu nyingi duniani Afrika ikiwa na mfano halisi.
"Pamoja na mazingira haya nawasihi msivunjike moyo wala kukata tamaa, masuala ya kisheria hayabadiliki kwa siku moja yanahitaji kupitia hatua kadhaa na kila jambo linaweza kupatiwa ufumbuzi hasa wadau wote watakaposhirikiana na kujenga hoja zenye ushawishi na tija kwa pande zote" alisisitiza Habimana.
Naye Lily Liu ambaye ni mjumbe kutoka shirika la ICNL aliahidi kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika nyanja zote ili kufanikisha na kutimiza adhma ya kuwa na jamii isiyo na sheria kandamizi zinazoathiri dhana nzima ya uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari.
No comments: