LIVE STREAM ADS

Header Ads

Salamu za Umoja wa Watemi wa Usukuma

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

UMOJA WA WATEMI WA USUKUMA S.L.P. 76 BUJORA MWANZA.
SALAMU MAALUM KWA SHEREHE YA BULABO NA KWA MGENI RASMI MHESHIMIWA DR. HAMISI  KIGWANGALA, WAZIRI MALIASILI NA UTALII.

Awali ya yote nakupongeza kwa kuitikia wito wa mwaliko wa kuja kuumua mambo yafuatayo;
1). Uhai wa sherehe hizi za kufurahia mavuno ya kila msimu wa mwaka kwa jamii na wenyeji ya Kanda ya Ziwa wa kabila la wasukuma.

2). Mheshimiwa mgeni rasmi, Kituo cha Utamaduni cha Bujora na Umoja wa Watemi wa Usukumani wa Kanda ya Ziwa ni Hifadhi ya kudumisha uishi salama wa utamaduni wa mila na jadi za Ubuntu. Ubuntu wa wenyeji asilia wa kabila la wasukuma. Sherehe hizi zina umri wa miaka zaidi ya 50.

3). Maonyesho ya wasanii wa kabila la wasukuma ni ngao na kinga ya kifikra ya kuzuia vizazi vipya kuwa mateka wa ulevi wa utamaduni potofu. Yaani utamaduni potofu wa kujengwa na malimwengu ya utandawazi ya miiko ovu dhidi ya mila na jadi za utamaduni wa uafrika wetu.

4). Mheshimiwa Mgeni Rasmi;
a). Serikali inalinda miti asilia na inalinda viumbe adimu wasitoweke.

b). Vile vile Serikali katika Mbuga za Serengeti na kwingineko wanalinda Faru, Tembo, Simba na wanyama wengineo wasitoweke.

5). Tanzania je? Ni nani wanalinda na kuhifadhi mila na Jadi za Utamaduni wa Ubuntu – yaani ujamii wetu usitoweke? Je jawabu sahihi ni kwamba ulinzi wa uhifadhi na usalama kwa uishi hai wa mila na jadi za utamaduni wetu, Je? Ni kuenziwa Tuzo na Tunu za mfumo wa Utemi wa kila eneo la kila wilaya na kila Mkoa?

6). Mheshimiwa Mgeni rasmi; Kwa kuwa kila fursa ina mlango wake na ina mlezi wake, kwa hiyo sasa nashawishika kukuomba uwe mlezi wa kukaribisha neema za kurutubisha ustawi na maendeleo ya Kituo cha Bujora cha Utamaduni.

7). Mheshimiwa Mgeni Rasmi; Nakuomba utumie vipaji vyako uwe ni chachu ya kuboresha mazingira ya Kituo hiki cha Bujora. Kituo hiki ndiyo kitambulisho pekee cha kuhifadhi historia kwa watafiti wa mambo ya kale na kwa masomo ya kuhusu mambo ya Utamaduni wa Mila na Jadi za wenyeji wa ardhi hii waitwao wasukuma.

8). Mheshimiwa Mgeni Rasmi;
a). Kituo hiki cha Bujora na Umoja wa Watemi wa Usukumani huunda majawabu ya kutoa fafanuzi za kuhusu kuongoza werevu wa kutamadunisha mawazo ya vizazi vipya. b)Hivyo vizazi vipya tunapenda vienzi na kuuishi utamaduni asilia wa msemo wa kazi wa Mhe. Rais Dr. John P. Magufuli “HAPA KAZI TU” kwa kisukuma husema kwamba:- “UYO UDUMA HANG’WAKWE YUCHAHO’ maana yake; asiye fanya kazi ya kuunda familia yake familia huteketea.

9). Mheshimiwa Mgeni Rasmi; a)Napenda tena kutumia fursa hii kukupongeza kwa kitendo chako cha kuja kujenga mwendelezo wa uhai wetu wa Jumuiko la Umoja wa Watemi wa Tanzania.

b). Naomba kukuarifu kwamba Watemi wana motisha wenye ari na wenye stamina na wenye morali wa ari ya upendo mkubwa kwa Mhe. Rais Dr. John P. Magufuli.

10). Mheshimiwa Mgeni Rasmi; Nakuomba umpelekee salamu za shukrani Mhe. Rais Dr. John P. Magufuli za kutoka katika Imani kubwa za Uongozi wa Kituo hiki cha Bujora cha Utamaduni. Vile vile mpe salamu za kumtakia heri na afya njema za kutoka katika Umoja wa Watemi wa usukumani na za kutoka kwa Umoja wa Watemi wa Tanzania.

11). Mheshimiwa Mgeni Rasmi; a)Kwa kuwa Imani ni zawadi ya Mwenyezi Mungu na ni mzizi unaootesha matunda ya kila jema. Kwa hiyo sasa kwa kuwa Hekima huongoza busara, na kwa hiyo sasa Umoja wa Watemi wa Tanzania unapongeza Hekima za Mhe. Rais Dr. John P. Magufuli.

b). Mhe. Rais Dr. Magufuli anaongoza Dira ya Ukombozi kwa Ustawi na Maendeleo ya Jamii Uchumi na Taifa kwa Hekima za Uzalendo na kwa maongozo ya busara za Tunu za Utaifa. Watemi tunasema hongera sana kwa Uongozi bora wa kwako Mhe. Rais Dr. John P. Magufuli.

12). Mheshimiwa Mgeni Rasmi; Mhe Rais Dr. John P. Magufuli mpe salamu za ujumbe ufuatao wa kutoka kwa Umoja wa Watemi wa Usukumani;

- Duniani ukishindanisha mbio za ukweli zishindane na mbio za Uongo – mbio za Uongo hufika mapema zaidi ya mbio za ukweli. Lakini mwambie kwamba; Ndoana ya mvuvi bila chambo haivui samaki, Watanzania wana macho na wana akili zisizo na ulemavu wa hisia za kutambua mali halisi na mali bandia zilizopo sokoni. Tunamtakia heri katika kazi zake zote.

13). Mheshimiwa Mgeni Rasmi a)Mcheza ngoma hutuzwa, tunaomba upokee zawadi ya Umoja wa Watemi wote waliojumuika hapa katika hii sherehe ya Bujora ya mwaka huu 2019. b)Zawadi yetu kwako ni dua za kukutakia mafanikio makubwa katika wito wako wa kutumia wananchi wa Jimbo lako la Nzega Vijijini na Taifa letu la Tanzania.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi Wahenga husema kwamba chafya ya mpishi haizimi moto wa jikoni. Kwa kuwa wewe ni kaa la moto mtu akilikanyaga ataungua, kwa hiyo sasa, Mungu mwingi wa Rehema akujalie Tuzo zake katika safari yako ya duruzu za Kisiasa za mwaka 2020?
Mungu mwingi wa rehema akujalie Tuzo zake. Amen. Ahsante kwa kunisikiliza.
Ndimi,

ya mvuvi bila chambo haivui samaki, Watanzania wana macho na wana akili zisizo na ulemavu wa hisia za kutambua mali halisi na mali bandia zilizopo sokoni. Tunamtakia heri katika kazi zake zote.

13). Mheshimiwa Mgeni Rasmi
a). Mcheza ngoma hutuzwa, tunaomba upokee zawadi ya Umoja wa Watemi wote waliojumuika hapa katika hii sherehe ya Bujora ya mwaka huu 2019.

b). Zawadi yetu kwako ni dua za kukutakia mafanikio makubwa katika wito wako wa kutumia wananchi wa Jimbo lako la Nzega Vijijini na Taifa letu la Tanzania.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi Wahenga husema kwamba chafya ya mpishi haizimi moto wa jikoni. Kwa kuwa wewe ni kaa la moto mtu akilikanyaga ataungua, kwa hiyo sasa, Mungu mwingi wa Rehema akujalie Tuzo zake katika safari yako ya duruzu za Kisiasa za mwaka 2020?

Mungu mwingi wa rehema akujalie Tuzo zake. Amen. Ahsante kwa kunisikiliza.
Ndimi,
John Shibuda
Ng'wanasandala- Mtemi Mteule wa Nela- Kwimba
Mratibu Mkuu wa Umoja wa Watemi wa Usukuma
Jumatatu Juni 24, 2019
Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.