LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kampeni ya "Shinyanga ya Kijani" yafana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com 
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa), Kheri James amezindua rasmi kampeni ya Shinyanga ya Kijani inayolenga kuwaandaa vijana wa chama hicho kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini mwishoni mwaka huu 2019.

Uzinduzi huo ulifanyika leo Juni 19, 2019 katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa ndani na nje ya Mkoa Shinyanga. 

"Huu ni mkakati wa kuwaandaa vijana wanachama wa CCM kote nchini kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nchini, kwa hiyo vijana wote wanaandaliwa kwa maana ya kuwaarifu kwamba mwaka huu uchaguzi utakuwepo" alisema James.

Alieleza kuwa mkakati huo unalenga kuwataarifu kuwa vijana wanalo jukumu la kujiandikisha katika madaftari ya wapiga kura kwenye maeneo yao na kujitokeza kugombea na kuwapigia kura wale watakaogombea pamoja na kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki na sheria za uchaguzi zinazingatiwa ili uchaguzi wetu uwe ni wa amani. 

"Leo nimepata heshima ya kuzindua mkakati huu katika Mkoa Shinyanga, imani yangu ni kwamba vijana leo tunawatangazieni kwamba uchaguzi mwaka huu upo,lakini nyinyi kama wananchi wengine mnayo fursa ya kugombea sawa na wengine, ili mpate haki hiyo lazima mjiandikishe ili mpate uhalali wa kuwa wananchi wakazi kwenye maeneo utakapofanyika uchaguzi" alifafanua.

Aidha aliwataka vijana walioaminiwa na kupewa nafasi za uongozi watambue kuwa kuwa wameaminiwa kwa maslahi ya umma hivyo watumike kwa maslahi ya umma huku akiwataka vijana wanaopewa madaraka na kujifanya siagi na kuyeyuka zama zao zinahesabika akidai hakuna cheo kinachodumu. 

"Tunahitaji kuwa wamoja, kushikana na kufanya kazi, mwana CCM popote alipo ana jukumu la kuendelea kukijenga chama, kuwatumikia watanzania wenzetu kwa hali na mali ili mwisho wa siku ustawi wa Watanzania na taifa kwa ujumla viweze kupatikana na niwakumbushe tu kazi ya kuimarisha chama inaendelea kote nchini" alisema. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Zainab Telack alieleza kuwa vijana wa CCM mkoani humo wapo imara na kwamba watahakikisha kuwa CCM inapata ushindi kila eneo na kwamba Serikali itahakikisha kuwa Demokrasia inazingatiwa ili uchaguzi uwe huru na wa haki.

Naye Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele ambaye pia ni Kaimu Rais wa Bunge la Afrika (PAP), aliwasihi vijana kuwa na nidhamu na wavumilivu na kuwataka wana CCM kupendana na kushirikiana huku akisisitiza kuwa CCM itashinda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu. 

"Mwaka huu tutatimiza miaka 20 tangu Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere afariki dunia, nataka niwaombe Jumuiya ya Vijana tujiandae kikamilifu kufikia mwezi Oktoba, na mimi nitatoa ushirikiano wote tushangilie maisha aliyoishi Baba wa Taifa, yapo mambo matatu aliyapigania ambayo ni umaskini, maradhi na ujinga hao maadui bado tunao, naomba tuendelee kupigana na maadui hawa" alisema Masele. 
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Kheri James akivishwa skafu alipowasili katika Ofisi ya CCM mkoani Shinyanga.Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Kheri James akipokelewa na vijana wa CCM alipowasili katika Ofisi ya CCM mkoani Shinyanga.Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Kheri James, akiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Shinyanga, Baraka Shemahonge (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Shinyanga, Mabala Mlolwa kuelekea katika Ofisi ya CCM Mkoa Shinyanga.Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Kheri James akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele.


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Kheri James akizungumza kwenye kampeni hiyo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Kheri James
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Kheri James akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Zainab Telack.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya Kijani.


Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James akiimba pamoja na msanii Beka Boy (kulia) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Wanachama wa CCM wakicheza na kupiga picha wakati wasanii Papii Kocha na Beka Boy.
Wasanii Papii Kocha na Beka Boy wakitoa burudani. 
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Kheri James akiimba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya Kijani. 
Diwani kutoka Nzega, ambaye pia ni msanii wa nyimbo za asili, Madebe Jinasa (katikati) akitoa burudani wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Imeandaliwa na Kadama Malunde, Malunde 1 Blog

No comments:

Powered by Blogger.