LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanawake wahimizwa kutowanyanyasa wanaume

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Katibu Tawala (RAS) Mkoa Iringa, Happynes Seneda (katikati waliosimama mstari wa mbele), akiwa katika picha ya pamoja na Wanawake Wafanyabiashara Masokoni wa jijini Dar es Salaam waliokuwa katika ziara ya mafunzo na kuwahamasisha wanawake wenzao wa Mkoa huo kujiunga na umoja wa kitaifa mjini humo mwishoni mwa wiki. Ziara hiyo iliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uingereza.
Afisa Biashara wa Manispaa ya Iringa, Benjamin Nyigu (katikati waliosimama mstari wa mbele), akiwa katika picha ya pamoja na Wanawake Wafanyabiashara Masokoni wa jijini Dar es Salaam waliokuwa katika ziara ya mafunzo na kuwahamasisha wanawake wenzao wa mkoa huo kujiunga na umoja wa kitaifa mjini humo. Ziara hiyo iliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uingereza.
Wanawake Wafanyabiashara Masokoni wa jijini Dar es Salaam wakiingia Ofisi ya Meya Manispaa ya Iringa.
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa EfG, Penina Reveta akimkabidhi, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe taarifa fupi ya shughuli zilizofanywa na shirika hilo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe (katikati waliosimama mstari wa nyuma), akiwa katika picha ya pamoja na Wanawake Wafanyabiashara Masokoni wa jijini Dar es Salaam waliokuwa katika ziara ya mafunzo na kuwahamasisha wanawake wenzao wa Mkoa huo kujiunga na umoja wa kitaifa mjini humo mwishoni mwa wiki.
Wanawake Wafanyabiashara Masokoni wa jijini Dar es Salaam wakitembela Soko la Mashine Tatu katika Manispaa ya Iringa.
Mwezeshaji Sheria Jane Nyanda kutoka Soko la Buguruni akizungumza na wanawake wa Soko la Mashine Tatu.
Mwenyekiti wa Soko la Mashine Tatu, Jafari Sewando, akizungumza na wanawake wa Soko hilo.
Picha ya pamoja na Wanawake wa Soko la Mashine Tatu.
Mwanasheria wa EfG akizungumza na wanawake wa Soko Kuu la Mkoa wa Iringa.
Afisa Tathmini na Uwajibikaji wa EfG, Samora Julius (kulia), akizungumza na wanawake wa Soko Kuu la Mkoa wa Iringa mwishoni mwa wiki wakati katika mkutano wa uhamasishaji wanawake wafanyabiashara wa soko hilo kujiunga na Umoja wa Kitaifa.
Mwenyekiti wa muda wa Umoja wa Wanawake Wafanyabiashara Masokoni Kitaifa, Betty Mtewele, akizungumza n wanawake wa Soko Kuu la Mkoa Iringa wakati akiwahamasisha kujiunga na umoja wa kitaifa.
Katibu wa Soko Kuu la Mkoa wa Iringa, Hamis Msimbe akizungumza.
Picha ya pamoja Soko Kuu la Mkoa wa Iringa.
Afisa Utawala wa EfG, Eva Buhembo akizungumza na wanawake wa Soko la Kihesa.
Mwenyekiti wa Soko la Kihesa katika Manispaa ya Iringa, Subira Mohammed.

Na Dotto Mwaibale, Iringa
Wanawame mkoani Iringa wametakiwa kuacha tabia ya kuwanyanyasa wanaume baada ya kupata mafanikio ya kifedha kupitia shughuli zao mbalimbali ikiwemo za kiujasiriamali.

Rai hiyo imetolewa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakati wakizungumza na timu ya wafanyabiashara wanawake kutoka Dar es Slaam ambao walikuwa kwenye ziara ya mafunzo na kufanya mchakato wa wafanyabiashara wanawake masokoni kuunda Umoja wa Kitaifa kupitia Shirika la Equality for Growth (EfG).

Katibu Tawala (RAS) wa Mkoa Iringa, Happynes Seneda aliwaomba wanawake hao kutosahau wajibu wao kwa waume zao baada ya kupata mafanikio ya kifedha.

"Mkifanikiwa kutokana na biashara zetu msiache majukumu yenu kwa waume zenu mimi mwenyewe hapa mnapo niona nina mtoto mchanga licha ya kuwa na majukumu mengi ya kiofisi nikifika nyumbani lazima nifanye majukumu yote ya familia yangu" alisema Seneda.

Seneda alitoa shukurani kwa EfG kwa kufika katika mkoa huo kwa lengo la kuwaunganisha wanawake wafanyabiashara masokoni ili wawe na nguvu ya maendeleo katika kujiinua kiuchumi.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe kwa nyakati nyingine naye alisisitiza wanawake wa mkoa huo kuacha tabia hiyo ya kuwanyanyasa wanaume pale wanapokuwa wamepata mafanikio na akatumia nafasi hiyo kulikaribisha shirika hilo kufanya kazi zake katika manispaa ya Iringa.

Katika hatua nyingine Mtunza Hazina wa Soko la Kihesa Venance Msigwa naye alirudia kuwaomba wanawake mkoani humo kuacha tabia ya kuwadharau na kuwanyanyasa wanaume pale wanapokuwa wamepata mafanikio.

Afisa Tathmini na Uwajibikaji wa EfG, Samora Julius alisema wamefanya ziara katika masoko tisa ya jiji la Mbeya ambayo ni Soweto, Uyole, Nzovwe, Ilomba, Mabatini, Igawilo, Iyunga, Soko Matola na Uhindini kwa lengo la kuwahamasisha wafanyabiashar wanawake katika masoko kuunda umoja wa kitaifa utakao wasaidia kwa mambo mbalimbali na kuelezea mafanikio ya Mradi wa Sauti ya Mwanamke Sokoni ambao umefadhiliwa na Ubalozi wa Uingereza.

Alisema katika mkoa wa Iringa wametembelea masoko matatu yaliyopo ndani ya manispaa ambayo ni Mashine Tatu, Soko Kuu na Soko la Kihesa ambapo kwa mikoa yote miwili ya Mbeya na Iringa kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wafanyabiashara hao wanawake masokoni kujiunga na umoja huo kitaifa.

No comments:

Powered by Blogger.