LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ni vyema Mwongozo wa Uwekezaji ukachapishwa kwa Kiswahili- TPSF

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye amekiri kwamba ni vyema mwongozo wa uwekezaji maarufu kama “Blue Print” ukachapishwa na kusambazwa kwa lugha ya Kiswahili ili kutoa fursa kwa wafanyabiasha wengi nchini kuusoma na kuuelewa.

Simbeye ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano wa majadiliano baina ya sekta binafsi Kanda ya Ziwa uliofanyika leo Julai 07, 2019 jijini Mwanza ukihusisha washiriki kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita na Kagera.

Mkutano huo ni mfululizo wa mikutano minane inayotarajiwa kufanyika katika Kanda nane nchini ili kutoa fursa kwa wadau wa sekta binafsi kutoa maoni yatakayosaidia kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini na hivyo kuondoa vikwazo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa. 
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara na Viwanda (TCCIA) Mkoa Mwanza, Joseph Kahungwa akizungumza kwenye mkutano huo.
Mfanyabiashara Kheri Amran kutoka jijini Mwanza akitoa maoni yake kwenye mkutano huo.
Mfanyabiashara Pili Makunenge kutoka mkoani Kagera akitoa maoni yake kwenye mkutano huo.
Mtaalam wa mazingira bora ya biashara nchini, John Mduma akiwasilisha mada kuhusu Mwongozo wa Uwekezaji Tanzania (Blue Print) kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Godfrey Simbeye (kulia), Mwenyekiti wa TPSF Salum Shamte (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa Mwanza, Joseph Kahungwa (kushoto) wakifuatilia mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Wadau wa sekta binafsi Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mkutano huo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.