Header Ads

Wadau wa Sekta Binafsi Kanda ya Ziwa watoa maoni yao kuhusu "Blue Print"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imewakutanisha wafanyabiashara kutoka mikoa mitano ya Kanda ya Ziwa ili kujadili na kutoa maoni yao kuhusu namna ya kuboresha mwongozo wa uwekezaji maarufu kama “Blue Print” unaolenga kuondoa vikwazo vya biashara na uwekezaji nchini.

Mkutano huo wa majadiliano baina ya wadau wa sekta binafsi umefanyika leo Julai 10, 2019 jijini Mwanza ukiwa ni mkutano wa pili baada ya ule uliofanyika jijini Dodoma Mei 20, 2019 ambapo jumla ya mikutano minane inatarajiwa kufanyika katika Kanda nane nchini ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara kutoa maoni yatakayosaidia kuondoa vikwazo vya biashara na uwekezaji.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye akizungumza kwenye mkutano huo.
 Mfanyabiashara jijini Mwanza, Kheri Amran akitoa maoni yake kwenye mkutano huo.
 Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.