LIVE STREAM ADS

Header Ads

Makonda atangaza mamilioni kwa wananchi na waendeshaji wa mitandao ya kijamii

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza na waandishi wa mitandao ya Kijamii.

Na Dotto Mwaibale
Mamilioni ya Shilingi yametengwa na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda kama zawadi kwa ajili ya waandishi wa habari watakao shinda shindano la kuwauliza maswali wananchi kuhusu Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Akizungumza ofisini kwake leo, Makonda alisema shindano hilo litawahusu waandishi wa habari wanao endesha mitandao ya kijamii kama vile Online TV, Blog, Twitter, Website, Facebook na Instagram.

Alisema maswali yatakayoulizwa ni 12 ambayo yameandaliwa na ofisi yake ambapo mwandishi mshindi kwa kuuliza atajinyakulia kitita cha Shilingi Milioni tatu huku mwananchi atakayejibu vizuri akipata Shilingu 100,000.

Alisema kuwa maswali mengine 12 yatabuniwa na waandishi wenyewe lakini yanatakiwa yawe yenye mvuto na kusisimua na mshindi wa eneo hilo atajinyakulia Shilingi Milioni tatu na mwananchi atakaye yajibu kiufasaha atapata Shilingi 100,000.

"Maeneo litakapofanyika shindano hili ni sehemu za bar, saluni, kwenye vijiwe vya waendesha bodaboda, masokoni na kwa wamachinga ambapo waandishi watawauliza maswali mbalimbali ya jinsi wanavyoijua SADC na watakaojibu kwa usahihi watajinyakulia kiasi hicho cha fedha" alisema Makonda akibainisha kwamba baada ya mahojiano hayo kila mwanahabari atayarusha hewani kwa kutumia mtandao wake.

Makonda alisema mshindi wa kwanza wa shindano hilo atapata Shilingi Milioni tatu, mshindi wa pili Milioni mbili na mshindi wa tatu Milioni moja na kwamba sherehe ya kukabidhi fedha hizo kwa washindi itafanyika Agosti 05, 2019 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es salaam.

Shindano ili linafanyika ikiwa ni moja ya hatua ya hamasa kuelekea kwenye mkutano mkuu wa SADC ambao unatarajiwa kufanyika hapa nchini hivi karibuni ambapo utaongozwa na Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

No comments:

Powered by Blogger.