Wafanyabiashara waliokimbia Tanzania watakiwa kurejea
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amewakaribisha wafanyabiashara
ndani na nje ya nchi kutumia fursa ya usafirishaji mizigo kupitia Ushoroba wa
Kati (Central Corridor) unaohusisha njia ya reli na bandari.
Mhandisi
Kamwelwe ameyasema hayo leo Julai 30, 2019 wakati akizungumza kwenye hafla ya usafirishaji wa
mabehewa ya mizigo kwa kutumia meli ya MV. Umoja kupitia Ziwa Victoria kutokea
bandari ya Mwanza Kusini (Tanzania) hadi bandari ya Portbell (Uganda),
uliofanyika katika bandari ya Mwanza Kusini.
Kwa mara ya
kwanza safari ya usafirishaji mizigo ilizinduliwa Juni 24, 2018 ikiwa ni miaka
10 tangu isitishwe katika bandari ya Mwanza Kusini (Tanzania) hadi bandari ya
Portbell (Uganda) ambapo hatua hiyo tayari imeanza kuleta tija ya gharama nafuu
kwa wanaosafirishaji.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments: